Baba amdunga bintiye kisu kwa ugomvi kuhusu taa Mombasa

Katika mabishano hayo, mwanamume huyo anadaiwa kuokota kisu cha jikoni na kumchoma bintiye kabla ya kutoroka eneo la tukio.

Muhtasari
  • Mashahidi na mamlaka walifichua kuwa kisa hicho cha kusikitisha kilisababishwa na ugomvi wa taa inayoweza kuchajiwa na jua, kufuatia kukatika kwa umeme kwa muda katika eneo hilo.
Mwanamke mjamzito apatikana amedungwa visu mgongoni
Mwanamke mjamzito apatikana amedungwa visu mgongoni
Image: Maktaba//The Star

Kwa sasa polisi wanamsaka baba mmoja anayeshukiwa kumuua bintiye wakati wa ugomvi wa kinyumbani eneo la Changamwe Mombasa.

Diana Yumbya, 25, alitangazwa kufariki alipofika katika Hospitali ya Bomu baada ya kudungwa kisu kifuani usiku wa manane mnamo Juni 1, kulingana na ripoti za polisi.

Mashahidi na mamlaka walifichua kuwa kisa hicho cha kusikitisha kilisababishwa na ugomvi wa taa inayoweza kuchajiwa na jua, kufuatia kukatika kwa umeme kwa muda katika eneo hilo.

Katika mabishano hayo, mwanamume huyo anadaiwa kuokota kisu cha jikoni na kumchoma bintiye kabla ya kutoroka eneo la tukio.

Majirani waliosikia mtafaruku huo walimkimbiza mwanamke huyo hospitalini ambapo ilitangazwa kuwa amefariki alipofika.

Polisi walifika hospitalini hapo na kuufanyia kazi mwili huo ambao ulikuwa na jeraha la kuchomwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Silaha hiyo ilipatikana kutoka eneo la tukio, polisi walisema.

Mshukiwa huyo alipatikana Jumapili huku kukiwa na msako dhidi yake, polisi walisema na kuongeza kuwa wanachunguza mauaji katika tukio hilo.

Wakati huo huo, watu wawili walifariki tofauti katika ajali za barabarani katika eneo hilo.