Tazama maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Jumatano- KPLC

KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo

Muhtasari

•KPLC ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Migori, Nyeri, Meru, Kiambu, Mombasa na Kakamega.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Juni 5.

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Migori, Nyeri, Meru, Kiambu, Mombasa na Kakamega.

Katika kaunti ya Migori, baadhi ya sehemu za maeneo ya Rongo, Kanga, na Kokuro zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kiawara, Belle View, Nairutia, Wangata, Matopeni, na Mar zitakosa umeme kati tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kagaene, Kibuline, na Mioponi katika kaunti ya Meru zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kiambu, sehemu kadhaa za maeneo ya Karanjee, Nyatarangi, Murera Sisal, Juja Farm na mji wa Limuru zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Mombasa, baadhi ya sehemu za maeneo ya Umoja, Kongowea, Kengeleni, na Kisauni zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu kadhaa za maeneo ya Muduma, Ingotse na Bushiri katika kaunti ya Kakamega pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.