KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Alhamisi

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Juni 6.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, West Pokot, Nyeri, Busia, Kiambu, na Mombasa.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Juni 6.

Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, West Pokot, Nyeri, Busia, Kiambu, na Mombasa.

Katika kaunti ya Nairobi, mtaa wa Garden Estate na baadhi ya viunga vyake vitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Makutano, Kapenguria, Murkwijit, Safari Hotel, Kamatira, na Kesogon katika kaunti ya West Pokot zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tano asubuhi.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kamatogu, Honi Resort, Mwireri, Jersey Farm, na Aberdare County Club katika kaunti ya Nyeri zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Busia, baadhi ya sehemu za maeneo ya Butula na Bumutiru zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi  na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za Tola, Bob Harris, Ngoingwa, Metro, TIBS, na Compuera katika kaunti ya Kiambu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu kadhaa za maeneo ya Msumarini, Vipingo na Junju katika kaunti ya Mombasa pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.