KPLC yatangaza maeneo ambayo yataathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Jumatatu

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Juni 10.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Baadhi ya sehemu za Lang'ata Road zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Juni 10.

Katika taarifa ya siku ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na  Nairobi, Bomet, Kisii, Nyeri, Murang'a, Homa Bay na Kiambu.

Katika kaunti ya Kiambu, baadhi ya sehemu za Lang'ata Road zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Koiwa, Cheptalal, na Siomo katika kaunti ya Bomet zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kegati, na Rianyamwamu katika kaunti ya Kisii zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Homa Bay, sehemu kadhaa za maeneo ya Kawonda na Andiwo zitakosa umeme kati saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Thunguma, na Meeting Point katika kaunti ya Nyeri zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kahaini na Bendor katika kaunti ya Murang'a zitakosa umeme kati ya saa tatu  asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kiambu, sehemu kadhaa za maeeneo ya Kenyatta Road, Kagwe, na Pascha zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.