DCI yapata magari 5 yaliyoibiwa, wamkamata mshukiwa mkuu

Tukio hilo lilirekodiwa na maafisa wa upelelezi wa Buruburu na magari yote yalivutwa hadi Kituo cha Polisi cha Buruburu pamoja na mshukiwa.

Muhtasari
  • Wapelelezi hao walieleza zaidi kuwa mkuu wa kikundi cha wizi wa magari amekuwa akitumia nyumba yake kama mahali pa kuhifadhi na kupotosha mwonekano wa magari yaliyoibiwa.
DCI yapata magari 5 yaliyoibiwa, wamkamata mshukiwa mkuu
Image: DCI/ X

Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Jumatatu asubuhi, walifukua maficho huko Kamulu ambapo magari matano yaliyokuwa yameibwa yalikuwa yamefichwa.

Katika taarifa iliyotolewa na DCI mnamo Jumatatu, wapelelezi hao walieleza kuwa walivamia nyumba ya mshukiwa mkuu huko Kamulu, ambayo mshukiwa alikuwa akiitumia kama maficho.

Wapelelezi hao walieleza zaidi kuwa mkuu wa kikundi cha wizi wa magari amekuwa akitumia nyumba yake kama mahali pa kuhifadhi na kupotosha mwonekano wa magari yaliyoibiwa.

Huku wakifanyia kazi ripoti ya kijasusi kutoka makao makuu ya Nairobi, DCI Buruburu na maafisa wa polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Kamulu, wapelelezi  hao walifanikiwa kumkamata mshukiwa huyo.

"Kwa kuzingatia upelelezi, wa CRIB kutoka Hqs za Mkoa wa Nairobi, DCI Buruburu na maafisa wa KPS kutoka Kituo cha Polisi cha Kamulu walielekea Kamulu kando ya Barabara ya Josna katika makazi ya Kiura (mshukiwa), ambapo gari lililoripotiwa kuibiwa lilipatikana likiwa katika harakati za kubomolewa, soma taarifa hiyo kwa sehemu.

Zaidi ya hayo, maafisa hao walisimulia kuwa moja ya gari lililopatikana katika uvamizi wa asubuhi liliripotiwa kuibwa katika eneo la Umoja Innercore baada ya mmiliki kukuta halipo muda mfupi baada ya kuliegesha.

Magari mengine, yaliyopatikana ni pamoja na Mazda Demio ya bluu Toyota Ractis (silver), Suzuki Mira (silver) na Toyota Passo nyeupe.

Kulingana na DCI, gari hilo aina ya Toyota Passo ambalo awali lilikuwa na rangi ya buluu, lilikuwa limebadilishwa na kuwa nyeupe na tayari kuuzwa tena.

Tukio hilo lilirekodiwa na maafisa wa upelelezi wa Buruburu na magari yote yalivutwa hadi Kituo cha Polisi cha Buruburu pamoja na mshukiwa.