KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo, Jumatano

Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Muhtasari

•Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. 

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Meru, Murang'a, Nyeri, Nyamira, na Homa Bay.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Juni 19. 

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Meru, Murang'a, Nyeri, Nyamira, na Homa Bay.

Katika kaunti ya Nairobi, eneo la KCC Village litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kisumu na Chiga katika kaunti ya Kisumu yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Green Wood Mall na Charia katika kaunti ya Meru zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Murang'a, baadhi ya sehemu za maeneo ya Ngararia na Kandara zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Nyaga, Oaklands, na Kahuguini katika kaunti ya Kiambu zitakosa umeme katy ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Nyeri, baadhi ya sehemu za maeneo ya Ihururu na Mathari zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Chebilat na Kijauri katika kaunti ya Nyamira  zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za Kalamindi na Wachara katika kaunti ya Homa Bay ziliathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.