Azimio yataka IG Koome kujiuzulu pamoja na mkuu wa polisi wa Nairobi

Wawili hao walifeli katika majukumu yao ya kuwalinda wakenya kwa amani waliokuwa wakiandamana kupinga mswada wa fedha wa 2024-Kalonzo

Muhtasari

•Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amemtaka inspekta jenerali wa polisi,Japhet Koome kujiuzulu pamoja na mkuu wa polisi wa Nairobi ,Adamson Bungei.

•Wawili hao wameponzwa baada ya kushindwa kuwalinda wakenya kufuatia kifo cha Rex aliyeuawa kwa kupigwa risasi.

KALONZO MUSYOKA
Image: HISANI

Viongozi wa muungano wa upinzani wa Azimio  walitoa wito wa kujiuzulu mara moja kwa  Inspekta Jenerali wa polisi Japhet Koome na mkuu wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei kufuatia mauaji ya Rex Masai.

Kwenye mahojiano na wanahabari,Ijumaa 21, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alibainisha kuwa wawili hao walifeli katika majukumu yao ya kuwalinda wakenya kwa amani waliokuwa wakiandamana kupinga mswada wa fedha wa 2024.

Kalonzo pia  alimtaka mkurugenzi wa taasisi ya mashtaka kuwafungulia mashtaka Koome, Bungei na afisa wa polisi aliyehusika na mauaji ya Rex.

"Kama Azimio na kwa niaba ya wananchi, tunamtaka inspekta jenerali Japheth Koome na mkuu wa mkoa wa Nairobi Bw. Adamson Bungei watoe taarifa zao za kujiuzulu mara moja kwa kushindwa kuwalinda waandamanaji hao kwa amani. Pia tunamtaka mkurugenzi wa mashtaka kumfungulia mashtaka Koome. , Bungei, na maafisa wao walaghai kwa mauaji ya Rex," taarifa hiyo ilisomeka.

Mwanasiasa huyo wa Azimio alihoji kwa nini maafisa wa polisi walichukua hatua kali dhidi ya waandamanaji ambao hawakuwa na silaha na wasio na vurugu. Waliomba haki itendeke na wakataka afisa aliyehusika afikishwe mahakamani.

"Hili ni tukio la kusikitisha na matokeo makubwa. Muungano wetu umefadhaishwa sana na mauaji ya Rex. Tuna kumbukumbu nyingi sana za misiba hii, na mawazo na maombi yetu ni pamoja na familia yake, marafiki, na jamii ambayo imeteseka. hasara kubwa kama hii..." Kalonzo alisema.

Aidha,Kalonzo aliahidi kusimama na familia ya marehemu Rex hadi haki ipatikane wakitafuta majibu kufuatia kisa cha jana,Alhamisi 20 kwenye maandamano.

Rex aliuawa kwa maandamano baada ya kupigwa risasi na afisa wa polisi.