Patrick Quarcoo astaafu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Africa Group baada ya miaka 24

"Nilipoanzisha Kundi la Radio Africa mwaka wa 2000, maono yangu yalikuwa kuunda jukwaa ambalo lingeweza kufahamisha, kuhamasisha, na kuunganisha watu kote nchini Kenya na bara," Quarcoo alisema.

Muhtasari

• Quarcoo aliwashukuru wafanyakazi wa Radio Africa Group kwa usaidizi wao na kujitolea kwa miaka yote ambayo amekuwa katika kampuni hiyo akisema walisajili ukuaji mkubwa.

• Kwa timu yake ya wasimamizi, Quarcoo alisema anajivunia kile walichofanikiwa pamoja.

Patrick Quarcoo.
Patrick Quarcoo.

Mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji Patrick Quarcoo ameondoka Radio Africa Group baada ya miaka 24 ya huduma.

Quarcoo aliondoka kwenye kampuni Jumatano, Julai 24 katika memo iliyotumwa kwa wafanyikazi.

"Nilipoanzisha kampuni ya Radio Africa mwaka wa 2000, maono yangu yalikuwa kuunda jukwaa ambalo lingeweza kufahamisha, kuhamasisha, na kuunganisha watu kote nchini Kenya na bara," Quarcoo alisema.

"Ninapostaafu, Radio Africa Group inaingia katika awamu muhimu ya safari yake. Mpito huu unatoa fursa ya kipekee kwa kampuni kulainisha mikakati yake, ikilenga ufanisi wa gharama, kuongeza faida na mipango yetu ya maudhui."

Quarcoo aliwashukuru wafanyakazi wa Radio Africa Group kwa usaidizi wao na kujitolea kwa miaka yote ambayo amekuwa katika kampuni hiyo akisema walisajili ukuaji mkubwa.

"Tumekua kutoka kituo kimoja cha redio hadi kampuni iliyostawi yenye Vituo sita vya ushawishi na zaidi ya transmita 40 kote nchini Kenya, na kupanuka hadi nchini Nigeria, gazeti na uwepo mkubwa wa kidijitali," alisema.

"Nina imani kwamba timu mpya ya uongozi itaendesha mabadiliko yanayohitajika kwa ari na dhamira ile ile ambayo tumekuwa tukishikilia kila wakati. Wana tajiriba ya kutosha  kupeleka kampuni mbele, na kutumia msingi wetu thabiti kufikia mafanikio makubwa zaidi."

Kwa timu yake ya wasimamizi, Quarcoo alisema anajivunia kile walichofanikiwa pamoja.

"Ubunifu yenu, uthabiti, na kujitolea imekuwa nguvu inayosukuma mafanikio yetu. Ninawahimiza kukumbatia sura hii mpya kwa shauku sawa na kujitolea kwa ubora," alisema.

Wakati huo huo aliwapongeza wateja wa matangazo ya biashara kwa usaidizi wao usioyumbayumba na ushirikiano kwa miaka mingi.

"Imani yenu kwa Radio Afrika kama mshirika wa masoko imekuwa muhimu katika ukuaji wetu. Tunapopitia kipindi cha mpito, tunatarajia kuendelea na ushirikiano wetu, kutoa suluhu za kiubunifu zinazokidhi mahitaji yako yanayoendelea."

"Asanteni nyote kwa kuwa sehemu ya safari hii ya ajabu. Nawatakia kila la heri katika nyakati za kusisimua zinazokuja."

Mhariri: Davis Ojiambo.