Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa mitetemeko wa ardhi

Ikiwa uko kitandani, geuza uso chini na kufunika kichwa na shingo yako kwa mto.

Muhtasari

•Mtetemeko wa ardhi ulishuhudiwa jijini Nairobi usiku wa Jumanne Julai  16,2024 huku wengi wakijawa na hofu.

•Hii si mara ya kwanza Kenya kushuhudia mtetemeko wa ardhi.

Image: HISANI

 Mtetemeko wa ardhi ulishuhudiwa jijini Nairobi na viunga vyake usiku wa Jumanne mwendo wa saa mbili unusu usiku,wengi wakijawa na hofu.

Hii si mara ya kwanza Kenya kushuhudia mtetemeko wa ardhi.

Mwaka wa 2007, Kenya na Tanzania zilipata matetemeko saba ya ardhi katika muda wa siku tano.

Tetemeko lililokumbukwa zaidi lilisikika mnamo Julai 12, 2007, na ukubwa wa 4.4 kwenye Kiwango cha Richter. Mitetemeko ya ardhi yaliyofuata yalifikia kipimo cha sita.

Kulingana na ripoti, maeneo tofauti ya nchi yamekuwa yakikumbwa na matetemeko ya ardhi kila mwaka tangu 2017.

Tetemeko la ardhi la juu zaidi katika miaka ya hivi majuzi lililorekodiwa lilikuwa Agosti 12, 2020, huko Mombasa, likiwa na kipimo cha 6.0 kwenye Kipimo cha Richter, huku la chini kabisa lilirekodiwa mnamo Februari 25, 2021, Nairobi, 4.2 kwenye Kipimo cha Richter.

                              Zingatia haya ikiwa kuna mtetemeko wa ardhi;

  •Kila wakati hakikisha kuwaangalia watu wanaoishi na ulemavu, kwani hawawezi kusonga kama watu wenye uwezo.

  •Ikiwa uko kwenye gari, weka breki yako ya maegesho na usubiri hadi mtetemeko uishe  ,washa redio kwa taarifa za dharura za matangazo.

  •Ikiwa uko kitandani, geuza uso chini na kufunika kichwa na shingo yako kwa  mto.

  •Ikiwa uko ndani, kaa ndani na usikimbie  nje au kwenye vyumba vingine wakati wa tetemeko la ardhi.Kuna uwezekano mdogo wa kujeruhiwa ikiwa utaendelea kukaa hapo ulipo.

 •Ikiwa uko kwenye uwanja au ukumbi wa michezo, kaa kwenye kiti chako. Kinga kichwa na shingo yako kwa mikono yako au kwa njia yoyote iwezekanavyo.

                           Vyanzo

https://www.ready.gov/earthquakes

https://www.cdc.gov/natural-disasters/about/index.html