Kaunti 8 kuathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Jumatatu- KPLC

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Agosti 5.

Muhtasari

•KPLC imesema baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

• Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Bomet, Nandi, Kakamega, Homa Bay, Embu, Kirinyaga, na Murang'a.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Agosti 5. 

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Bomet, Nandi, Kakamega, Homa Bay, Embu, Kirinyaga, na Murang'a.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu ya mtaa wa South C itaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Kapset na Kimulot katika kaunti ya Bomet yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu za eneo la Mlango katika kaunti ya Nandi zitakosa umeme kati ya saa nne asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu za eneo la Musanda katika kaunti ya Kakamega zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Ndhiru, Opinde na Obuya katika kaunti ya Homa Bay yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Kivwe, Kevote na Ndatu katika kaunti ya Embu yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.

 Katika kaunti ya Kirinyaga, maeneo ya Karira, Ndorome na Marura yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Makuyu, Kirimiri na Ndithini katika kaunti ya Murang'a pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.