Kampuni ya Telegramu sasa itatoa baadhi ya data za watumiaji kwa mamlaka

Maelekezo hayo yatatolewa kwa mamlaka zilizo na vibali vya kufanya upekuzi au maombi mengine halali ya kisheria.

Muhtasari

•"Mabadiliko ya masharti yake ya huduma na sera ya faragha "yanapaswa kuwakatisha tamaa wahalifu", CEO Pavel Durov alisema.

•Waendesha mashtaka walimshtaki CEO Pavel Durov kwa kuwezesha shughuli za uhalifu kwenye jukwaa.

Image: BBC

Programu ya kutuma ujumbe ya Telegram imesema itakabidhi nambari ya kipekee ya utambulisho inayotolewa kwa kila kifaa kilichounganishwa kwenye mtandao kwa mamlaka zilizo na vibali vya kufanya upekuzi au maombi mengine halali ya kisheria.

Mabadiliko ya masharti yake ya huduma na sera ya faragha "yanapaswa kuwakatisha tamaa wahalifu", Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Pavel Durov alisema katika ujumbe wake wa Telegraph siku ya Jumatatu.

"Ingawa 99.999% ya watumiaji wa Telegraph hawana uhusiano wowote na uhalifu, 0.001% wanaohusika katika shughuli za uhalifu wanatengeneza taswira mbaya kwa jukwaa zima, na kuweka masilahi ya karibu watumiaji wetu bilioni hatarini," aliendelea.

Tangazo hilo linaashiria mabadiliko makubwa kwa Bw Durov, mwanzilishi mwenza wa jukwaa hilo mzaliwa wa Urusi ambaye alizuiliwa na mamlaka ya Ufaransa mwezi uliopita katika uwanja wa ndege kaskazini mwa Paris.

Siku kadhaa baadaye, waendesha mashtaka huko walimshtaki kwa kuwezesha shughuli za uhalifu kwenye jukwaa.

Madai dhidi yake ni pamoja na kushiriki katika kueneza picha za unyanyasaji wa watoto na biashara ya dawa za kulevya.

Pia alishtakiwa kwa kushindwa kufuata sheria.

Bw Durov, ambaye amekanusha mashtaka hayo, alikashifu mamlaka muda mfupi baada ya kukamatwa, akisema kuwa kumshikilia ili kuwajibika kwa uhalifu uliofanywa na wahusika wa tatu kwenye jukwaa la Telegram ni jambo la "kushangaza" na "kupotosha."

Wakosoaji wanasema Telegramu imekuwa kitovu cha habari potofu, ponografia ya watoto, na maudhui yanayohusiana na ugaidi kwa sababu ya kipengele kinachoruhusu vikundi kuwa na hadi wanachama 200,000.

Ukilinganisha na jukwaa la WhatsApp inayomilikiwa na Meta, inaweka mipaka ya ukubwa wa vikundi hadi watu 1,000.