Sehemu za kaunti ya Murang'a kukosa umeme leo, Jumamosi- KPLC

KPLC imesema baadhi ya maeneo ya kaunti ya Murang'a yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Muhtasari

•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika sehemu kadhaa za eneo la Mlima Kenya siku ya Jumamosi, Septemba 28.

Katika taarifa ya Ijumaa jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti ya Murang'a yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. 

Sehemu za maeneo ya mji wa Murang'a na Kabuta ni baadhi ya ambako huduma za umeme zitaathirika.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Mukuyu na Maragi zikiwemo soko la Mukuyu, Stanley Haven, Murang'a High School na viunga vyao pia zitashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.