Fahamu maeneo ya Kenya ambako hakutakuwa na stima leo, Novemba 2

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi,Nyandarua, Kilifi na Mombasa.

Muhtasari

•KPLC ilitangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti 4 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni

•Kukatizwa kwa umeme katika maeneo yaliyotajwa kumepangwa kwa sababu ya shughuli za matengenezo zitakazokuwa zikifanyika.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi.

Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti 4 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi,Nyandarua, Kilifi na Mombasa.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za eneo la Riverside zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Aidha, sehemu za mtaa wa Westlands na Parklands Rd zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane alasiri.

Sehemu za mtaa wa Tudor katika kaunti ya Mombasa zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni siku ya Alhamisi.

Wakati huo huo, sehemu za maeneo ya Kokotoni na Jimba katika kaunti ya Kilifi yatashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Nyandarua, mji mzima wa Engineer utaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

KPLC imeeleza kuwa kukatizwa kwa umeme katika maeneo yaliyotajwa kumepangwa kwa sababu ya shughuli za matengenezo zitakazokuwa zikifanyika.