Inawezekana!Makau avunja kimya huku kura za urais zikiendelea kuhesabiwa

IEBC ndilo shirika pekee lililo na mamlaka ya kujumlisha na kutangaza matokeo ya urais.

Muhtasari
  • Makau avunja kimya huku kura za urais zikiendelea kuhesabiwa
Makau Mutua
Makau Mutua

Msemaji wa Azimio La Umoja Makau Mutua amevunja ukimya wake kuhusu kujumlisha kura za urais zinazoendelea.

Mutua, katika taarifa yake siku ya Alhamisi, alisema kuwa atawafahamisha  Wakenya iwapo jambo litatokea.

"Baadhi ya watu wanashangaa kwa nini Msemaji wa Azimio haongei. Uwe na uhakika kwamba anafanya kazi kwa bidii. Anapokuwa na jambo la kusema, atafanya hivyo. Kwa sasa, hebu sote tuangalie, tufuate, na tuhakikishe kinachoendelea," aliandika

Aliwataka Wakenya na wafuasi wa Azimio kusalia na matumaini huku mchakato wa kujumlisha kura ukiendelea.

Kambi ya Azimio mnamo Alhamisi ilitayarisha kituo chake cha mawasiliano katika KICC huku muungano huo ukiripotiwa kupanga kukutana na wawaniaji wake waliofaulu.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka imeanza kupokea na kuthibitisha fomu za matokeo ya uchaguzi wa urais kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi wa maeneobunge.

Wakenya walipiga kura mnamo Agosti 9 kuchagua serikali mpya.

IEBC ndilo shirika pekee lililo na mamlaka ya kujumlisha na kutangaza matokeo ya urais.

Hata hivyo, tume iliruhusu vituo vya habari kufanya mchakato wao wa kujumlisha na kuhesabu kura.

Katika taarifa nyingine msemaji huyo wa Azimio alisema kwamba kila jambo linawezekana.