Kauli 10 za kukumbukwa kutoka kwa Malkia Elizabeth II

Malkia Elizabeth wa 2 alifariki jana akiwa na umri wa miaka 96.

Muhtasari

• "Kila mtu ni jirani yetu, haijalishi ni kabila gani, imani au rangi gani," – 2004.

Malkia Elizabeth 2
Malkia Elizabeth 2
Image: BBC NEWS

Malkia wa Uingereza, Elizabeth wa pili alifariki usiku wa Alhamis akiwa na umri wa miaka 96, baada ya kuhudumu kama malkia wa ikulu ya Buckingham kwa miaka 70, kumfanya kuwa mtu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi.

Baada ya kifo chake, sasa ni rasmi kwamba mwana wa mfalme, Charles wa tatu atachukua hatamu rasmi kama mfalme.

Katika kusherehekea maisha yake aliyoishi vizuri kwa miongo tisa na ushee, Radiojambo.co.ke tumechukua muda kuangalia baadhi ya nukuu na matamshi ya kukumbukwa ambayo malkia Elizabeth wa pili aliwahi nukuliwa akisema katika kipindi cha uongozi wake tangu mwaka 1953 hadi 2022 umauti ulipomfika.

1. “Kuna matatizo mengi mazito na ya kutisha katika nchi hii na ulimwenguni lakini hayatatatuliwa hadi kuwe na amani katika nyumba zetu na upendo mioyoni mwetu," Malkia alisema katika matangazo yake ya Krismasi – 1986.

 

2. "Lakini tusijichukulie kwa uzito sana, Hakuna hata mmoja wetu aliye na ukiritimba wa hekima na lazima tuwe tayari kusikiliza na kuheshimu maoni mengine." – 1991.

3. "Kila mtu ni jirani yetu, haijalishi ni kabila gani, imani au rangi gani," – 2004.

4. "Kuzaliwa kwa mtoto huleta furaha kubwa - lakini basi harakati ya kumkuza huanza." – 2006.

5. "Maisha yanapoonekana kuwa magumu, wajasiri hawalali chini na kukubali kushindwa; badala yake, wanaazimia zaidi kupigania maisha bora ya baadaye." – 2008.

6. "Inafaa kukumbuka kuwa mara nyingi ni hatua ndogo, sio mikurupuko mikubwa, ambayo huleta mabadiliko ya kudumu zaidi," – 2019.

7. "Tunaweza kushikilia maoni tofauti lakini ni wakati wa mfadhaiko na ugumu ambao tunahitaji kukumbuka kuwa tuna mengi zaidi sawa kuliko yanavyotugawa." – 1974.

8. "Sote tunahitaji kupata uwiano sawa kati ya hatua na kutafakari. Pamoja na vikwazo vingi, ni rahisi kusahau kusitisha na kutathmini," – 2013.

9. "Labda tunafanya mambo mengi sana yasiyo sahihi na machache sana ya yaliyo sawa. Shida ya utusitusi ni kwamba inajilisha yenyewe na unyogovu husababisha huzuni zaidi."

10. "Ingawa tunaweza kufanya matendo makuu ya wema, historia inatufundisha kwamba wakati mwingine tunahitaji kujidhibiti kutoka kwetu - kutoka kwa uzembe wetu au uchoyo wetu.