DP Rigathi: Ninawashukuru watu wa Mathira kwa kusimama nami

Aliongeza kuwa Serikali ya Kitaifa itashirikiana na uongozi wa Jimbo hilo ili eneo hilo liwe na hadhi yake ya awali.

Muhtasari
  • Anawaelezea wapiga kura kuwa watu maalum, akisema imani yao na msaada wao kwake, ulifanya ndoto zake kuwa kweli
Naibu Rais William Ruto
Image: TWITTER// RIGATHI GACHAGUA

Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa shukrani zake kwa wakazi wa Mathira kwa kusimama naye licha ya dhiki alizopata.

Anawaelezea wapiga kura kuwa watu maalum, akisema imani yao na msaada wao kwake, ulifanya ndoto zake kuwa kweli.

"Kwa namna ya pekee kabisa, nataka kuwashukuru watu wa Mathira ambapo safari yangu ya kisiasa ilianzia... Mambo yalipozidi kuwa magumu na mfumo wa haki ya jinai ulipowekwa silaha dhidi yangu. Watu wa Mathira walinishikilia," alisema.

Alizungumza alipotembelea afisi za NGCDF kwa hafla ya kukabidhi madaraka eneo bunge.

Mbunge huyo wa zamani wa Mathira alisema wapiga kura walimtia moyo kupitia masaibu hayo na kumwambia asilazimishwe kuachana na azma yake ya kuwa DP.

"Hivyo ndivyo nilivyoweza kuchukua msimamo thabiti. Laiti watu wa Mathira wangeyumba na kuamua kwa sababu nilikuwa nimezingirwa na miradi ilikuwa inasitishwa na kutelekezwa, sitakuwa hapa nilipo," alisema.

"Kwa hivyo ninashukuru sana."

Gachagua aliahidi kuwazawadia.

"Nitashukuru milele na ninataka kuwahakikishia kuwa nitakuwa hapa kila wakati na chochote ninachoweza kuwafanyia watu wa Mathira, nitafurahi sana kuwafanyia," alisema.

Aliongeza kuwa Serikali ya Kitaifa itashirikiana na uongozi wa Jimbo hilo ili eneo hilo liwe na hadhi yake ya awali.