Aisha Jumwa abubujikwa na machozi wakati wa mahojiano

Ndoa ya mapema iliningoja kwa mikono miwili, nikawa mama wa mzaliwa wangu wa kwanza. Hii ni moja ya mila ambayo lazima idhibitiwe."

Muhtasari
  • Ndoa ya mapema iliningoja kwa mikono miwili, nikawa mama wa mzaliwa wangu wa kwanza. Hii ni moja ya mila ambayo lazima idhibitiwe."
AISHA JUMWA
Image: EZEKIEL AMING'A

Waziri Mteule wa Utumishi wa Umma, Jinsia na Affirmative Action Aisha Jumwa,alibubujikwa na machozi mbele ya jopo la bunge huku akisimulia safari yake ya maisha.

Jumwa mwenye hisia kali aliambia jopo la mchujo lililoongozwa na Spika Moses Wetangula jinsi wazazi wake walivyotatizika kumlisha yeye pamoja na ndugu zake wengine 27.

Huku akibubujikwa  na machozi, mbunge huyo wa zamani wa Malindi alisema alilazimishwa kuoleka akiwa na umri mdogo baada ya kuacha shule nane kutokana na ukosefu wa karo.

“Wazazi wangu walikuwa maskini, walikuwa wakihangaika kunipatia riziki mimi na ndugu zangu wengine 27,” alisema.

"Nilisoma shule ya msingi kuanzia 1983 hadi 1991 ambapo niliacha shule kwa kukosa karo. Nilikuwa nyumbani na hakukuwa na matarajio kabisa ya kupanua upeo wangu

Ndoa ya mapema iliningoja kwa mikono miwili, nikawa mama wa mzaliwa wangu wa kwanza. Hii ni moja ya mila ambayo lazima idhibitiwe."

Baadaye alisajiliwa kufanya  KCSE mnamo 2011.

. "Nilipopoteza uchaguzi, nilitafakari na kukagua. Nilirejea shuleni na kukamilisha KCSE 2011. Niliendelea hadi JKUAT alifuzu kwa Utawala 2022."

Alipata pia Shahada za Uzamili katika Uongozi Mkuu mnamo 2015.

Kamishna huyo wa zamani wa PSC alisema ana thamani ya Sh100 milioni.