Miguna Miguna afichua sababu kuu ya kwenda Kisumu Ijumaa

Miguna alikuwa tayari ametangaza Jumanne kwamba atazuru nyumbani kwake.

Muhtasari
  • "Kwenda nyumbani, haswa kwa mtu aliyehamishwa kwa nguvu kwa miaka 5, sio kitendo cha vita. Ni kitendo cha amani, urejesho wa kihemko na kimwili," alisema.
Jenerali Miguna hatimaye ametua nchini
Jenerali Miguna hatimaye ametua nchini
Image: Andrew Kasuku

Wakili Miguna Miguna anatazamiwa kuzuru nyumbani kwake Kisumu siku ya Ijumaa baada ya kurejea kutoka Kanada alikokuwa uhamishoni kwa lazima.

Miguna alisema itakuwa ziara ya heshima kwani hajakutana na familia yake kwa muda mrefu.

"Kwenda nyumbani, haswa kwa mtu aliyehamishwa kwa nguvu kwa miaka 5, sio kitendo cha vita. Ni kitendo cha amani, urejesho wa kihemko na kimwili," alisema.

Aliwasihi wapinzani wake wasitume wahuni wampige mawe kwani anaenda kuwaomboleza wanafamilia wake walioaga dunia alipokuwa hayupo.

"Tafadhali msiwahamasishe vijana wasio na ajira kunipiga mawe siku ya Ijumaa. Naenda kuomboleza wanafamilia wangu," alisema.

Miguna alikuwa tayari ametangaza Jumanne kwamba atazuru nyumbani kwake.

Katika taarifa yake, wakili huyo alisema atakuwa katika kijijini Kisumu Ijumaa, Oktoba 28.