Mwanaume ashinda bet, aficha uso wakati wa kuichukua ili mkewe asijue ni yeye

Mwanaume huyo alishinda bet ya shilingi bilioni 3.6 za Kenya,

Muhtasari

• Wakati wa kuchukua kitita chake, alitoka mwenyewe na kujifunika kwa gauni kama kibonzo alipokuwa anakabidhiwa pesa hizo.

Mwanaume ashinda bet ya kuficha sura mkewe asijue
Mwanaume ashinda bet ya kuficha sura mkewe asijue
Image: Bloomberg

Mwanaume mmoja kutoka China amegonga vichwa vya habari baada ya kuficha sura yake alipokwenda kuchukua kitika cha pesa alizoshinda katika mchezo wa bahati nasibu.

Mwanaume huyo alieleza kwamba aliamua kuficha utambulisho wa sura yake ili mkewe na watoto wake wasijue kama ni yeye kwani hakutaka familia yake ijue kama ashakuwa tajiri wa kubahatisha.

Kulingana na jarida la Bloomberg, mwanaume huyo kwa jina Li alishinda Yuan milioni 219 za Uchina ambazo ni sawa na shilingi bilioni 3.6 pesa za Kenya na wakati wa kuchukua kitita chake, alitoka mwenyewe na kujifunika kwa gauni kama kibonzo alipokuwa anakabidhiwa pesa hizo.

"Sikumwambia mke wangu na mtoto wangu kwa kuogopa kwamba wangeridhika sana na hawatafanya kazi au kufanya kazi kwa bidii siku zijazo," mwanamume huyo aliambia gazeti hilo wiki jana.

Alitoa yuan milioni 5 kwa shirika la usaidizi na akasema hakuwa hakuwa ameamua la kufanya na zingine.

Mwanamume huyo alinunua tikiti ya ushindi katika duka moja mjini Litang. Siku moja baada ya kugundua kuwa ameshinda, aliendesha gari hadi jiji kubwa kuwasilisha tikiti kwenye makao makuu ya bahati nasibu.

"Nililala tu hotelini kwa sababu niliogopa kutoka na kupoteza tikiti ya bahati nasibu," alisema.

Li ambaye amekuwa akicheza bahati nasibu kwa takriban muongo mmoja alisema huu ni ushindi wake mkubwa ingawa ameshinda mara kadhaa.

“Nilishinda yuan kadhaa tu hapo awali. Ninachukulia kununua bahati nasibu kama burudani, na familia yangu haijali. Zaidi, situmii pesa nyingi juu yake, na bahati nasibu hutoa mwanga wa matumaini kwangu,” mwanaume huyo alinukuliwa na vyombo vya habari Uchina.