Waume wa viongozi waliochaguliwa hawapaswi kufifia - Wamatangi

Alisema kuwa kuna majukumu yaliyoainishwa kwa wanawake wa viongozi lakini waume yanapuuzwa.

Muhtasari
  • Akiongea Alhamisi, Wamatangi alisema gavana wa Meru na mumewe bado wanaweza kwenda pamoja kwenye hafla kama wanandoa wanavyofanya
GAVANA KIMANI WAMATANGI

Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi ametofautiana na wazo kwamba wenzi wa viongozi waliochaguliwa wanapaswa kufifia.

Gavana huyo alikuwa akirejelea kisa cha Gavana wa Meru Kawira Mwangaza ambaye amekuwa kwenye vichwa vya habari kwa kumteua mwenzi wake Murega Baichu kuwa balozi wa Vijana wa kaunti hiyo.

Akiongea Alhamisi, Wamatangi alisema gavana wa Meru na mumewe bado wanaweza kwenda pamoja kwenye hafla kama wanandoa wanavyofanya.

"Kama mtindo wa Mwangaza na mumewe ulikuwa wa kufanya kila kitu pamoja, hiyo haipaswi kubadilika kwa sababu tu alichaguliwa. Tunafaa kuwaangalia viongozi wa kigeni wanaoenda na wenzi wao kwenye hafla kuu,” alisema kwenye mahojiano katika runinga ya Citizen.

"Kwa upande wa Barrack Obama hata alipokuwa akihutubia mikutano mikuu ya bunge, mke wake alikuwepo na hata angepata fursa ya kuhutubia taifa na hivyo ndivyo alivyofanya jina lake."

Alisema kuwa kuna majukumu yaliyoainishwa kwa wanawake wa viongozi lakini waume yanapuuzwa.

"Wanawake  wanatarajiwa kufanya mambo fulani, wanakaribishwa katika hafla na wanaheshimiwa lakini waume huwa wanapata upande mbaya zaidi," alisema.

Gavana alisema Wakenya wanafaa kuheshimu nafasi ya familia kwa viongozi waliochaguliwa.

Gavana wa Meru, hata hivyo, alikanusha madai ya kumwajiri mumewe.