Msikubali mahindi ya GMO-Ledama kwa Wakenya

Kulingana na Olekina, anahisi kuwa mahindi hayo si salama kwa matumizi ya binadamu

Muhtasari
  • Kauli hii ya waziri Kuria ya kuleta mahindi ya GMO nchini imechukuliwa vibaya na baadhi ya Wakenya na viongozi

Seneta wa kaunti ya Narok, Ledama Olekina ametuma ujumbe mzito kwa wakenya akidai kuwa hawafai kukubali hatua ya waziri wa Biashara na Viwanda Moses Kuria ya kuagiza mahindi ya GMO kwa muda wa miezi 6 ijayo nchini.

Kulingana na Olekina, anahisi kuwa mahindi hayo si salama kwa matumizi ya binadamu na hivyo huenda yakaleta madhara ambayo yanaweza kusababisha vifo.

"Ndugu Wakenya Msiruhusu mahindi ya GMO kuingia nchi hii tafadhali msiruhusu! Ikiwa katibu wa baraza la mawaziri anaweza kusema wameamua kwa makusudi kuruhusu GMO nchini kuua watu je kweli tutaingia kwenye mtego wao? come on be serious ... kichekesho kabisa!" Seneta Ledama Olekina alisema.

Kauli hii ya waziri Kuria ya kuleta mahindi ya GMO nchini imechukuliwa vibaya na baadhi ya Wakenya na viongozi wengine ambao wamedai wanapaswa kununua kwanza mahindi ya Kenya.

Ni kauli ambayo imeibua hisia mseto nchini,uku nchi ikikabiliwa na makali ya njaa.