Sonko atoa zawadi ya Ksh 400,000 kwa polisi atakaye wakamata washukiwa waliomtoa mtoto macho

Alitoa zawadi ya Sh400,000 kwa afisa yeyote atakayewatia nguvuni washukiwa wa kitendo hicho.

Muhtasari
  • Alivitaka vyombo vya usalama vinavyochunguza kisa hicho kutoacha jambo lolote lile
  • Okenyuri alisema hakuna mtoto anayestahili kuteswa, jinsi Sagini alivyoteseka mikononi mwa wahalifu wake
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Image: Facebook//Mike Sonko

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ameungana na viongozi wengine kulaani shambulio la Junior Sagini kutoka Ikuruma, Marani huko Kisii.

Sagini, mwenye umri wa miaka 3, aling'olewa macho wakati wa shambulio baya la majambazi wasiojulikana Alhamisi usiku.

Sonko alielezea tukio hilo kuwa la kuhuzunisha.

Alitoa zawadi ya Sh400,000 kwa afisa yeyote atakayewatia nguvuni washukiwa wa kitendo hicho.

Gavana huyo wa zamani pia aliahidi nyongeza ya Sh200,000 kwa mtu yeyote ambaye atajitolea habari ambazo zinaweza kusababisha kukamatwa kwa washukiwa wakuu.

Tukio hilo limeibua msururu wa hisia katika mgawanyiko wa kisiasa.

Seneta Mteule Essy Okenyuri alitembelea Sagini katika Hospitali ya Macho ya Kisii Jumamosi ambako anapokea matibabu.

Alivitaka vyombo vya usalama vinavyochunguza kisa hicho kutoacha jambo lolote lile.

Okenyuri alisema hakuna mtoto anayestahili kuteswa, jinsi Sagini alivyoteseka mikononi mwa wahalifu wake.

"Kila mtoto anastahili kutendewa kwa utu bila kujali mazingira anayolelewa. Natumai hakuna kitakachomzuia kwani haki inatafutwa kwake," alisema.

Mwanaharakati wa kisiasa Steven Nyarangi alisema kisa hicho kilikuwa cha kuhuzunisha moyo. Kufikia Jumamosi jioni, wapelelezi mjini Kisii walisema walikuwa wakimdadisi baba-Thomas Ongaga- kuhusu tukio hilo.

Alikuwa akiishi na mtoto huyo baada ya kutengana na mke.

Polisi, hata hivyo, walisema bado hayuko chini ya ulinzi wao kama mshukiwa na kuongeza kuwa walimtafuta kwa maelezo kama sehemu ya uchunguzi wa awali.