Tutamtafuta mpaka jela,'Sonko asema baada ya mshukiwa aliyeng'oa macho ya baby Sagini kukamatwa

Amewashukuru Esnah Nyaramba, Mhe Japho Nyakundi, Simba Arati, polisi, na timu yake ya Kisii kwa ushirikiano mzuri.

Muhtasari
  • Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko sasa amejitokeza kueleza maoni yake kuhusu kukamatwa kwa mshukiwa
Ochogo alipokuwa akisindikizwa kurejea katika seli ya polisi ya Rioma baada ya kufika mahakamani Jumatatu
Ochogo alipokuwa akisindikizwa kurejea katika seli ya polisi ya Rioma baada ya kufika mahakamani Jumatatu
Image: MAGATI OBEBO

Mvulana mwenye umri wa miaka mitatu kwa jina Junior Sagini sasa hana macho licha ya kwamba  alizaliwa na uwezo wake wa kuona.

Mvulana huyo alitekwa nyara katika eneo ambalo bado halijajulikana ambapo macho yake yalitolewa na baadaye akatupwa kwenye shamba la mahindi ambapo alipatikana baadaye.

Kumekuwa na uchunguzi unaendelea ni nani aliyemfanyia kijana mdogo kitendo hicho cha kinyama.

Baada ya uchunguzi wa muda mrefu, Maina Ochoki, binamu wa Sagini ambaye alikamatwa leo kama mshukiwa mkuu wa kitendo hicho cha ajabu, anatazamiwa kuzuiliwa kwa siku kadhaa akisubiri uchunguzi.

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko sasa amejitokeza kueleza maoni yake kuhusu kukamatwa kwa mshukiwa, Sonko anasema kuwa IPOA inafaa kufutiliwa mbali kwa sababu polisi wanapewa bunduki ili wasiharibu wahuni kama Ochoki lakini kuwaua papo hapo.

Mike Sonko anasema kuwa watamfuatilia hadi jela kwa sababu hakuna IPOA huko akiongeza kuwa lazima ahisi uchungu sawa na Sagini pia.

Amewashukuru Esnah Nyaramba, Mhe Japho Nyakundi, Simba Arati, polisi, na timu yake ya Kisii kwa ushirikiano mzuri.