Kericho: Spika awatupa nje wanahabari, bunge likijadili bajeti ya ziada

"Nani aliwaambia uje hapa? Toa wanahabari)hapa. Waache wafuatilie matukio mtandaoni" Spika aliwaamrisha walinda usalama.

Muhtasari

• "Nani aliwaambia uje hapa? Toa wanahabari)hapa. Waache wafuatilie matukio mtandaoni" Spika aliwaamrisha walinda usalama.

Bunge la kaunti ya Kericho lawafungia nje wanahabari
Bunge la kaunti ya Kericho lawafungia nje wanahabari
Image: Maktaba

Ijumaa alasiri bunge la kaunti ya Kericho lilikuwa na kikao maalum cha kujadili bajeti ya ziada ya matumizi ya kaunti hiyo.

Hata hivyo, tukio kubwa lilijili pale ambapo spika wa kaunti hiyo aliamuru wanahabari waliokuwa ange kunasa kikao hicho kwa kamera zao kutupwa nje ya majengo ya bunge ili wasipate kunasa kile ambacho kilikuwa kinajadiliwa na MCAs wa kaunti hiyo ya bonde la ufa.

Spika wa Kaunti Dkt Patrick Mutai alimwagiza Sajenti wa Arms kuwaondoa wanahabari wapatao 15 waliokuwa wameenda kuripoti kikao hicho. Walijumuisha wale kutoka Nation Media Group, Royal Media Services, Standard Media Group, K24 na waandishi wanaowakilisha vituo vya redio vya lugha za kienyeji.

"Nani aliwaambia uje hapa? Toa watu hao (vyombo vya habari) hapa. Waache wafuatilie matukio mtandaoni," spika Dkt Mutai aliwaambia maafisa wa usalama.

 Inaripotiwa kuwa awai wanahabari walikuwa wamealikwa kuhudhuria kikao hicho ili kuchukua habari lakini spika alibadili msimamo wake dakika za mwisho, jambo lililozua mvutano kiasi baina yake na naibu spika.

Wadadisi wa siasa za kaunti hiyo wanahisi kuwa kikao hicho huenda kikakumbwa na mabishano makali baina yamirengo miwili inayokinzana haswa kufuatia mabadiliko ya uongozi wa nyadhifa za bunge ambayo yalifanyika mwaka ukianza.

Wabunge 47 wa Bunge la Kaunti ya Kericho wanakutana tena takriban wiki moja baada ya mabadiliko ya uongozi wa Baraza kutekelezwa kwa mara ya tatu.