Utafiti: Asilimia kubwa ya watu wenye elimu hawamiliki nyumba

Ripoti ya KNBS ilisema 46.7% ya watu wanaomiliki nyumba hawana elimu rasmi huku 32.2% ya wasomi wakiwa ndio wamiliki.

Muhtasari

• Kwa ujumla, asilimia 45 ya wanaume wenye umri wa kati ya miaka 15 na 49 wanamiliki nyumba ikilinganishwa na asilimia 33 au chini.

Jumba la kifahari
Jumba la kifahari
Image: Maktaba,

Jumanne, shirika la kutoa takwimu nchini KNBS lilitoa takwimu za kushtusha katika masuala mbali mbali.

Moja ya takwimu ambazo zimeibua gumzo kali nchini ni ile iliyosema kuwa utafiti huo ulipata wanaume wengi ambao wanamiliki majumba ni wale ambao hawakuenda shule wala hawana elimu yoyote.

Utafiti huo ambao ulifanyika kati ya mwezi Februari na Julai mwaka jana ulionesha kuwa asilimia kubwa na wanaume walioshiriki katika utafiti huo na ambao walikubali kumiliki nyumba ni wale wasio na elimu ya darasani.

KNBS walisema kuwa asilimia 32.2 ambao wanamiliki nyumba ni wale wamesoma kupita kiwango cha kidato cha nne huku asilimia 46.7 ya wamiliki wa nyumba ni wale ambao hawana elimu ya darasani.

Mfano sawa unajitokeza kwa wenzao wa kike huku data ikionyesha asilimia 10 ya wamiliki wa nyumba ni wanawake wasio na elimu rasmi ikilinganishwa na asilimia 3 ambao wamepanda ngazi ya elimu ya juu.

Wadadisi na wataalamu wa mambo ya takwimu na sense wanahoji kuwa hili huenda linachangiwa na uhamaji kutoka mashambani kuelekea mijini ambapo wengi wa watu walio na elimu huamia mijini kutafuta kazi huku wasio na elimu wakisalia vijijini kujishughulisha na ukulima.

Kwa ujumla, asilimia 45 ya wanaume wenye umri wa kati ya miaka 15 na 49 wanamiliki nyumba ikilinganishwa na asilimia 33 au chini ya theluthi moja ya wanawake walio chini ya umri sawa.