(+PICHA)Kutana na mkewe na mwanawe George Magoha

Alianguka ndani ya nyumba yake. Alikimbizwa hospitali ambapo alitangazwa kuwa amefariki.

Muhtasari
  • Magoha alioa mkewe Dr Barbra Magoha, Mnigeria, na kwa pamoja walikuwa na mtoto mmoja Michael Magoha
MKEWE ALIYEKUWA WAZIRI WA ELIMU GEORGE MAGOHA,BABRA MAGOHA NA MICHAEL MAGOHA
Image: ANDREW KASUKU

Wakenya na familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu George Magoha wamo kwenye maombolezo kufuatia kifo chake Jumanne.

Magoha alioa mkewe Dr Barbra Magoha, Mnigeria, na kwa pamoja walikuwa na mtoto mmoja Michael Magoha.

Waziri huyo wa zamani wa Elimu alifariki katika hospitali ya Nairobi Jumanne akiwa na umri wa miaka 71.

Image: KWA HISANI

Alianguka ndani ya nyumba yake. Alikimbizwa hospitali ambapo alitangazwa kuwa amefariki.

Hospitali ya Nairobi katika taarifa ilithibitisha kifo chake.

MICHAEL MAGOHA
Image: ANDREW KASUKU

"Ni kwa masikitiko makubwa kwamba tunatangaza kifo cha ghafla na kisichotarajiwa cha Profesa George Magoha jioni hii katika Hospitali ya Nairobi," Mkurugenzi Mtendaji wa The Nairobi Hospital James Nyamongo alisema katika taarifa.

Viongozi tofauti wametuma rambirambi kwa familia wakiongozwa na Rais Ruto, kinara wa Azimio Raila Odinga miongoni mwa viongozi wengine.

MKEWE GEORGE MAGOHA,BABRA AKIWA KWENYE CHUMBA CHA KUHIFDHI MAITI CHA LEE
Image: ANDREW KASUKU