'Wakili wa jasho' Willis Otieno atoa msaada wa baiskeli kwa wanafunzi wa shule za kutwa

Wakili huyo aligonga vichwa vya habari kwa tamko lake la 'piki piki ponky paka mielo disco'

Muhtasari

“Baiskeli za Paka mielo kuendeshwa kurudi shuleni." - Wakili Otieno.

Wakili Otieno atoa msaada wa baiskeli shuleni
Wakili Otieno atoa msaada wa baiskeli shuleni
Image: Facebook

Willis Otieno, Wakili aliyegonga vichwa vya habari wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Agosti 2022 ametoa msaada wa baiskeli kwa wanafunzi wa shule za kutwa.

Wakili huyo kupitia ukurasa wake wa Facebook, alipakia picha akiwa anawapokeza wanafunzi hao wa shule za kutwa baiskeli kama njia moja ya kurahisisha usafiri wao kutoka nyumbani hadi shuleni na kurudi.

“Baiskeli za Paka mielo kuendeshwa kurudi shuleni. Kundi la kwanza la baiskeli zinazotolewa kwa watoto wa shule za sekondari za kutwa ili kuwezesha ufikiaji wa haraka wa shule. #MapemaNdioBest,” wakili huyo alisema.

Wakili huyo aligonga vichwa vya habari baada ya kuonekana akitoa wasilisho lako mbele ya jopo la majaji saba wa mahakama ya upeo huku akitiririkwa kijasho kutoka usoni na mashavuni.

Aidha, wakili Otieno ambaye alikuwa anawakilisha mlalamishi mmoja kwa jina David Kariuki ambaye alikuwa anapinga uhalali wa matokeo ya urais kutoka tume ya IEBC.

Katika wasilisho lake, Otieno huku akitokwa kijasho alisema kuwa ambacho aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati na makamishna wenzake walikifanya ni kucheza mchezo ambao ni wa zamani uliokuwa unachezwa na watoto kwa jin ‘pik pik ponky paka mielo disco’

Msemo huo ulienezwa zaidi nchini mpaka baadhi ya watu kuutumia kutengeneza muziki.

Produsa Motif alikuwa mmoja wa wabunifu waliotumia sauti ya Otieno akitamka maneno hayo na kuyaunganisha kwenye mdundo kama wimbo.