Nairobi: Kizaazaa mshukiwa wa ulaghai akizirai baada ya kukamatwa

Mshukiwa huyo alikuwa akiigiza kama afisa wa KDF na alikuwa akiwalaghai watu kuwa atawapa kazi katika jeshi la ulinzi.

Muhtasari

• Mwanamume huyo alikuwa akizurura karibu na barabara za Wangari Mathai akiwasubiri waathirika wake.

• Alikuwa amewahidi kuwapa kazi jeshini baada ya kumpa kiasi fulani cha pesa.

• Maafisa wa KFS walimshuku na kumkamata wakati alikuwa anapokezwa pesa kutoka kwa watu wawili waliotaka kuingia jeshini.

Mwanamume akiwa ametiwa pingu ndani ya seli.
Mwanamume akiwa ametiwa pingu ndani ya seli.
Image: Twitter

Kisa cha kushangaza kilishuhudiwa katika barabara ya Wangari Mathai jijini Nairobi baada ya mshukiwa wa ulaghai kuzirai alipokuwa anakamatwa na maafisa wa polisi.

Kulingana na taarifa kutoka kwa shirika la huduma kwa misitu nchini, mshukiwa huyo mwanamume alikuwa anawindwa na maafisa wa polisi kufuatia ripoti nyingi za kuwalaghai wananchi akiwaahidi kazi hewa, na alipokamatwa, alizirai ghafla.

Mwanamume huyo amekuwa akijifanay kuwa afisa mweney ushawishi katika jeshi la ulinzi KDF alikamatwa wakati alikwa amewaita watafutaji ajira wawili ambao kabla wampokeze pesa, maafisa wa polisi kutoka kitengo cha KFS kumrukia na kumweka chini ya ulinzi.

Baada ya kuzimia, alikimizwa hospitalini huku waathiriwa wawili waliokuwa wakimpokeza hongo kwa ajili ya kazi walikwepa pia.

“Hata hivyo alama zake ziliisha alipoonekana akizurura katika Makao Makuu ya KFS na walinzi wa KFS waliokuwa zamu. Baada ya kugundua kuwa gongo lake lilikuwa limepikwa, mwanamume huyo alizirai na kukimbizwa hospitali akiwa amepoteza fahamu huku wale aliowakusudia wakitoroka,” sehemu ya taarifa hiyo ilisoma.

Mwanamume huyo kwa sasa anaendelea kupata nafuu katika Hospitali ya Nairobi huku akiwa bado amekamatwa. Atafunguliwa mashtaka mahakamani punde tu atakapotoka hospitalini. Atashtakiwa kwa uigaji na kughushi.

Umma unashauriwa kuwa nafasi zinazotangazwa kwa ajili ya kuajiri ni kwa kuzingatia sifa na kwa mujibu wa maelezo ya kazi husika.