Mwanamke wa miaka 60 amfuma mumewe mkuki na kumuua baada ya kutaka mtoto

Richard Ssemambo mwenye umri wa miaka hamsini alikuwa akidai mtoto kutoka kwa mkewe mwenye umri wa miaka sitini.

Muhtasari

• Polisi pia walisema kuna madai kwamba Ssemambo aliwaua watoto wa Nanalongo (watoto wake wa kambo) wakati akitaka ampatie mtoto.

Crime Scene
Image: HISANI

Mwanamke mwenye umri wa miaka sitini aliyetambulika kama Nanlongo Babirye amemuua mumewe kufuatia matakwa kutoka kwake ya kupata mtoto.

Jarida moja la nchini Uganda liliripoti kuwa Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, Fred Enanga, mume wa Babirye ambaye tangu sasa ametambuliwa kama Richard Ssemambo mwenye umri wa miaka hamsini alikuwa akidai mtoto kutoka kwa mkewe mwenye umri wa miaka sitini.

Enanga alisema wanandoa hao waligombana na kutofautiana kuhusu suala hilo usiku wa kuamkia Jumamosi, Machi 4, 2023 katika eneo walilokuwa wamekwenda Kasangati, jarida hilo lilisema.

"Wanandoa hao walikuwa wameenda eneo la Kasangati walipotofautiana kuhusu kupata mtoto. Tumegundua kuwa mume Richard Ssemambo alikuwa akidai mtoto kutoka kwa mkewe mwenye umri wa miaka sitini,” Enanga alisema.

Aliongeza: “Wanandoa walipofika nyumbani, mke alipata mkuki na kumchoma mumewe. Nnalongo alimfunga tu kipande cha kitambaa mumewe jambo ambalo halikusaidia kwa sababu alivuja damu usiku kucha. Ssemambo alikutwa amekufa siku iliyofuata.”

Enanga pia alisema kuna madai kwamba Ssemambo aliwaua watoto wa Nanalongo (watoto wake wa kambo) wakati akitaka ampatie mtoto.

Alisema tangu wakati huo Nnalongo amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya shahada ya kwanza.

Enanga alifichua kuwa alikamatwa pamoja na watu wengine wanne wanaoishi katika eneo moja na yeye. Kwa mujibu wa Enanga, Nnalongo alikuwa land lady wa watu wanne aliokamatwa nao.

Wanne hao walikamatwa na kushtakiwa kwa kusaidia uhalifu.

"Tulikamata watu wengine wanne pamoja naye. Waliangalia tu uhalifu ukiendelea kumaanisha kuwa walisaidia uhalifu,” Enanga alinukuliwa.