Ushoga ni dhambi-Muhoozi asema huku akishauri mataifa ya Afrika

Jenerali huyo kutoka Uganda pia amesema kuwa ushoga ni kinyume na Biblia jinsi inavyofundisha.

Muhtasari
  • Muhoozi amefahamisha mataifa ya Afrika kwamba, kwa ujumla wake, anapendelea amani kuliko migogoro
KWA HISANI
KWA HISANI
Image: Muhoozi Kainerugaba

Jenerali Muhoozi Kainerugaba kwa mara uya kwanza ametoa maoni yake kuhusu uamuzi wa mahakama ya Kenya kuhusu LGBTQ.

Muhoozi Kainerugaba amechagua kutoa mwongozo kwa mataifa ya Afrika.

Kainerugaba ameshauri dhidi ya ushoga, akiitaja kuwa ni tabia ya dhambi.

Jenerali huyo kutoka Uganda pia amesema kuwa ushoga ni kinyume na Biblia jinsi inavyofundisha.

Hakuna kitu kitamu duniani, kulingana na jenerali wa Uganda, kuliko mwanamke.

Kulingana na Muhoozi, janga linakumba mataifa ya Afrika. Ameeleza kuwa hawezi kuruhusu ushoga katika bara la Afrika katika ushauri wake kama kamanda mkuu wa jeshi la Uganda.

Muhoozi amefahamisha mataifa ya Afrika kwamba, kwa ujumla wake, anapendelea amani kuliko migogoro.

Muhoozi anasisitiza kwamba bara la Afrika lina nguvu kweli kweli na kwamba baadhi ya mila, kama vile ushoga, hazifai kuvumiliwa.

"Kuna janga limezikumba nchi zetu... linaua watoto wetu. Kama Jenerali Mkuu wa Kiafrika, lazima niseme na kuwashauri. Ushoga ni DHAMBI! Mwenyezi Mungu aliwakusudia wanaume tu kwa wanawake na kinyume chake. Hakuna kitu kitamu zaidi ya mwanamke hapa duniani."