Hatuwezi kumruhusu Raila karibu na Ruto - Cherargei kwa Sakaja

Cherargei amemjibu Sakaja akidai kuwa Raila anafaa kuwa tayari kwa matokeo ya maandamano hayo.

Muhtasari
  • Awali alikuwa amefichua kuwa baadhi ya viongozi wa Kenya kwanza  hawataki umoja na kujumuishwa kwa viongozi wote katika ngazi ya kitaifa
Seneta wa Nandi, Samson Cherargei
Seneta wa Nandi, Samson Cherargei
Image: Facebook//Cherargei

Hisia za hivi majuzi za gavana wa Nairobi Johnson Sakaja zimefungua mazungumzo mapya katika ulingo wa kisiasa.

Awali alikuwa amefichua kuwa baadhi ya viongozi wa Kenya kwanza  hawataki umoja na kujumuishwa kwa viongozi wote katika ngazi ya kitaifa.

Sakaja alifichua kuwa Ruto anafaa kuwaalika viongozi wote wa kitaifa na kufanya mazungumzo nao kwani wana uungwaji mkono mkubwa ambao huenda ukavuruga nchi mara tu maandamano yatakapoanza.

Aliendelea kubainisha kuwa Nairobi itaathirika kwa vile ndio kitovu kikuu cha uchumi nchini.

Cherargei amemjibu Sakaja akidai kuwa Raila anafaa kuwa tayari kwa matokeo ya maandamano hayo.

Aliendelea kuangazia kuwa Ruto hatakuwa na mazungumzo naye kwani anashughulika kuhudumia nchi yake kusaidia kukabiliana na mfumuko wa bei wa bidhaa za kimsingi.

Cherargei amefichua kuwa serikali ya kitaifa haitamchukua yeyote kutoka Azimio katika nyadhifa za uteuzi.

"Salaaale ! @SakajaJohnson kwa hili umekosea ,Tinga HAITAKUWA karibu na mpendwa wetu H.E Ruto unaweza kuendelea na kufanya hendisheki/handcheque na Tinga PEKE YAKO kama ulivyofanya na masalio ya AZIMIO-OKA kule Kanairo. Tinga aanze kutafuta glucose ya Monday ile mbio inakuja ..."Cherargei alisema.