"Kwaheri mpenzi wangu!" Maneno ya mwisho ya mke kwa mumewe kabla ya kuchomwa moto

Wanakijiji wapatao 100 walivamia boma la mzee huyo wakimtuhumu mke wake, Mary Njoki, ajuza wa miaka 75 kuwa ni mchawi.

Muhtasari

• Mzee huyo kwa uchungu alikumbuka kwamba kabla ya kumtia kwenye tanuru, walimruhusu muda wa kuongea maneno ya mwisho na mumewe.

• Maneno yake ya mwisho yalikuwa ya uchungu kama yalivyokaririwa na mzee yule.

Mzee akilia kwa uchungu,
Mzee akilia kwa uchungu,
Image: Getty Images

Mzee mmoja kutoka kaunti ya Murang’a amehadithia kwa kumbukumbu za simanzi kisa kilichojiri nyumbani kwake siku moja jioni baada ya wanakijiji wenye ghadhabu kutimba nyumbani kwake wakiitaka damu ya mke wake.

Katika simulizi ambalo lilihadithiwa kwenye jarida moja la humu nchini, Mzee Kibaara alisema kwamba vijana waliojawa na ghadhabu walifika katika nyumba yake ya matope jioni moja wakitaka kumuua mke wake Mary Njoki mwenye umri wa miaka 75 kwa tuhuma za uchawi.

“Tulikuwa kwenye jiko letu la udongo ambalo liko nje ya nyumba yetu kuu…mke wangu alikuwa amemaliza tu kuandaa chai kwa ajili yetu. Tuliishi sisi wawili tu kwenye boma. Nilikuwa na maumivu ya yabisi magotini na nilikuwa nimeweka miguu yangu juu ya mawe mawili ya kupikia ili kupata joto huku nikinywa chai yangu,” Bw Kibaara anakumbuka.

Katika usiku huo wa maafa, wavamizi hao waliwakuta wameketi kando ya kila mmoja katika jikoni iliyo na taa ya bati.

"Jikoni lilijazwa na kupofusha taa nyingi za tochi ambazo kwa silika, nilidhani walikuwa maafisa wa polisi. Nilipofumba macho ili kuepusha athari chungu ya mwanga wa taa, nilisikia sauti ya kike ikipaza sauti kwa Kikuyu: Huyu hapa mchawi,” mzee huyo aliiambia Nation katika kijiji chake cha Kiamikoe eneo bunge la Kiharu.

Mzee huyo kwa mshtuko mkubwa, alifungua macho yake baada ya kusikia mke wake akizabwa kofi na mmoja kati ya vijana wale aliokisia idadi yao kuwa mia moja hivi.

Walimburura mkewe huku wakimtupia maneno kwamba muda wake wa kueneza ulozi katika kijiji hicho ulikuwa umefika mwisho.

Mzee alieleza kwamba silka yake ilimwambia kuwa ndiye anafaa kuwa mlinzi wa mkewe na hivyo alijisatiti na kuamka na ukuni huku akiwataka wote kumuachia mke wake na kuondoka kaitka boma lake.

Lakini maneno yake ya vitisho yalianguka kwenye masikio yaliyotiwa nta, kwani vijana wale hawakuwa tayari kumuachia mke wake.

Vijana wale waliendelea kumpiga mkewe huku wakimtaka kuwataja wote ambao walikuwa wanashirikiana nao katika uchao, kipigo ambacho kiliendelea kwa Zaidi ya saa mbili hivi.

Baadae walileta mataili ya magari na kuyatia moto tayari kumteketeza ajuza yule, lakini walimpa muda mchache kuzungumza na mumewe maneno ya mwisho.

“Kwaheri mpenzi wangu, wataniua bure ila kuwa na moyo dhabiti...nitakuwa nikikuangalia kutoka mbinguni,” mzee huyo alikariri maneno hayo ya mwisho kutoka kwa mke wake baina ya uchungu mwingi.