Miguna amtaka Raila kuomba Wakenya msamaha

Matamshi yake yalijiri punde tu baada ya Raila kutangaza kuwa Jumatatu, Machi 20, itakuwa siku ya mapumziko.

Muhtasari
  • Alisema kuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani kwa zaidi ya miaka 30 amekuwa akiwadanganya Wakenya, ndiyo maana anafaa kuomba msamaha kutoka kwao.
Image: TWITTER// MIGUNA MIGUNA

Wakili Miguna Miguna sasa anasema kuwa ni wakati wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kustaafu kutoka kwa siasa.

Kulingana na Miguna, Raila pia anafaa kutumia fursa hiyo kuwaomba Wakenya msamaha.

Alisema kuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani kwa zaidi ya miaka 30 amekuwa akiwadanganya Wakenya, ndiyo maana anafaa kuomba msamaha kutoka kwao.

"Staafu na uombe msamaha kwa miaka 30 ya usaliti, usaliti, fursa, woga na ujanja," Miguna alisema Jumatano.

Miguna ambaye wakati mmoja alikuwa mshauri wa Raila alipokuwa Waziri Mkuu ametokea kuwa mmoja wa wakosoaji wake wakubwa.

Matamshi yake yalijiri punde tu baada ya Raila kutangaza kuwa Jumatatu, Machi 20, itakuwa siku ya mapumziko.

Hii, alisema, ni kuruhusu wafuasi wa Azimio kusafiri ili kushiriki katika hatua kubwa dhidi ya kile alichokiita serikali haramu.

"Kwa hivyo sasa natangaza leo kwa jina la Azimio la Umoja One Kenya Alliance Coalition kwamba Jumatatu, Machi 20, itakuwa siku ya mapumziko," Raila alisema.