Aliwaacha watu wake baada ya hendisheki-Millicent Omanga amrushia vijembe Raila Odinga

Licha ya kushambuliwa kwenye mitandao ya kijamii Raila hajakata tamaa

Muhtasari
  • Aidha aliwaonya Wakenya kwa kumuunga mkono akidai kuwa aliwatelekeza watu wake baada ya hendisheki.
Seneta mteule Millicent Omanga
Seneta mteule Millicent Omanga
Image: TWITTER//MILLICENTOMANGA

Mapema leo, mwanasiasa maarufu Millicent Omanga alimshambulia Raila Odinga kwa mara nyingine tena.

Akichapisha kwenye ukurasa wake wa instagram, Omanga alifahamisha umma kwamba kila kitu ambacho Raila alikuwa akifanya kilikuwa kinamhusu yeye na washirika wake wa karibu.

Aidha aliwaonya Wakenya kwa kumuunga mkono akidai kuwa aliwatelekeza watu wake baada ya hendisheki.

Aligundua kuwa mtu pekee ambaye ni mkweli kuhusu Wakenya ni Ruto na kwa wakati ufaao kila mkenya atahisi athari za ukuaji wa uchumi.

"Yote ni kuhusu yeye na washirika wake wa karibu, akipangwa atatulia. Wewe shinda tu hapo unapiga sufuria na kijiko. Mnamo 2017, aliwaacha watu wake baada ya hendisheki Mtu pekee ambaye ni mkweli kuhusu Wakenya ni KK Govt. Kwa wakati ufaao kila Mkenya atahisi athari za ukuaji wa uchumi,"Omanga alisema.

Licha ya kushambuliwa kwenye mitandao ya kijamii Raila hajakata tamaa. Uamuzi wake unajiri baada ya rais William Ruto kukosa kutimiza lalama zake.

Hapo awali, kiongozi huyo wa azimio alikuwa amemtaka Ruto kutaja hatua za kupunguza gharama ya maisha na kufungua seva za tume huru ya uchaguzi na mipaka ili kuhakiki matokeo ya uchaguzi mkuu wa Agosti.

Raila alitoa wito wa kuchukuliwa hatua kubwa nchini na kufikia sasa amezuru kaunti tofauti akiwarai wafuasi wake kuhudhuria mkutano wa Machi 20 ili kueleza mshikamano katika harakati za kutafuta haki.