Ruto kuendelea kumuita Raila "my brother" ili kumaliza maandamano, nitaongeza "my dear"

Rais alisema yuko tayari kumbembeleza Odinga hata mara kumi kwa kuongeza "my dear brother" kama hilo litamaliza maandamano.

Muhtasari

• "Kama kumwita Raila Odinga my brother ndio kutasaidia awache maandamano, awache fujo, mimi nitamwita mara kumi" - Ruto.

Ruto aapa kuendelea kumuita Odinga "my brother" ili kumaliza maandamano
Ruto aapa kuendelea kumuita Odinga "my brother" ili kumaliza maandamano
Image: Facebook

Rais William Ruto ameapa kuendelea kumuita kiongozi wa upinzani Raila Odinga “ndugu yangu” hata Zaidi ya mara kumi kama hilo ndilo litamaliza maandamano.

Rais akizungumza wakati wa furari kwenye ikulu ya Nairobi jioni ya Jumatatu Aprili 17, alisema kuwa ako tayari kumubembeleza Odinga ili kumaliza maandamano na kuafikiana kuketi kwa mazungumzo.

Rais aliapa pia kuchagiza Zaidi hata kumuita “my dear” huku akisema kuwa wito wa maandamano kwa wafuasi wa Odinga unatishia biashara na uchumi wa taifa.

“Kama rais niliuliza my brother Raila Odinga kwamba tuwache maandamano. Tuwache fujo inaharibu mali ya watu, biashara ya watu, damu inamwagika. Nimeona tena wanalalimika mbona Ruto ameita Raila my brother angemwita mtu wa kitendawili. Wacha nirudie tena my brother Raila Odinga tuwache maandamano. Kama kumwita Raila Odinga my brother ndio kutasaidia awache maandamano, awache fujo, mimi nitamwita mara kumi hata nitaongeza my dear brother,” Rais alisema.

Rais alisema kuwa lengo kuu ni kusongeza taifa mbele kwa pamoja huku akisema yeye ndiye ametwikwa jukumu la kuongoza taifa kwa njia inayofaa.

“Sasa nah ii fuji yote ya kuharibu mali ya watu, unga utapungu bei namna gani?” Ruto aliuliza.

Mapema wiki jana, Odinga aliapa kurejelewa kwa maandamano huku mrengo wake ukijiandaa kwa mazungumzo ya pande zote mbili na mrengo wa serikali.

Odinga alisema maandamano yatafanyika sambamba na mazungumzo hayo, pindi tu baada ya mfungo wa mwzi mtukufu wa Ramadani kukamilika.