Hisia mseto baada ya Askofu Ole Sapit kudai kuna ukabila katika uteuzi wa ofisi za umma Serikalini

Ole Sapit pia alisema ubadhirifu wa rasilimali za umma umekuwa jambo la kawaida.

Muhtasari
  • Pia aliishutumu serikali kwa kupunguza kasi katika vita dhidi ya ufisadi.
  • Alisema mashirika ya serikali yanafaa kuhudumia Wakenya wote kwa usawa.

Askofu Mkuu wa Kianglikana Jackson Ole Sapit ameusuta utawala wa Rais William Ruto kuhusu kuongezeka kwa uhuni katika uteuzi wa ofisi za umma.

Katika taarifa yake, Sapit alisema uteuzi huo unaonyesha ukosefu wa uwajibikaji katika mashirika ya serikali.

Alisema mashirika ya serikali yanafaa kuhudumia Wakenya wote kwa usawa.

"Kuna ukabila mkali na urafiki, haswa kuhusu uteuzi wa umma. Kuna upungufu wa uwajibikaji na uwazi katika taasisi zetu. Hili halikubaliki," Ole Sapit alisema.

"Acha taasisi zote na mashirika ya serikali yawe na upendeleo na ufanisi, na sio tu kuonekana kwa ushawishi wa kisiasa, lakini kutumikia Wakenya wote bila upendeleo."

Askofu Mkuu alisema utawala mbovu daima umekuwa kichocheo cha mvutano wa kisiasa.

Pia aliishutumu serikali kwa kupunguza kasi katika vita dhidi ya ufisadi.

Ole Sapit pia alisema ubadhirifu wa rasilimali za umma umekuwa jambo la kawaida.

"Mivutano ya kisiasa inalisha utawala mbovu, na hakuna idadi ya mazungumzo yatakayoleta maelewano ikiwa serikali itafeli mtihani wa uwajibikaji. Tunaona kwamba serikali inapita njia inayoteleza kwa kulegeza kamba katika vita dhidi ya ufisadi," alisema.

"Kwa masikitiko yetu, kutokujali katika usimamizi wa rasilimali za umma na mambo ya umma kunazidi kuwa jambo la kawaida."

Wanaitandao walimshambulia Askofu huyo kwa matamshi yake, huku asilimia kuvbwa ikidai kwamba amekuwa mfuasi wa Rais Ruto, kwa hivyo hapaswi kuzungumzam lolote.