Mfahamu milionea ambaye anafanya kazi kwa bidii ili kubadili umri wake halisi

Alisema kuwa mtoto wake ana umri wa miaka 17 na anashindana naye na anataka wafanane na kiumri.

Muhtasari

•Mwanamume huyu ambaye ni mfanyabiashara anayejishughulisha na masuala ya teknolojia, anafanya jambo ambalo baadhi ya watu wameeleza kama kutaka kurudisha nyuma saa na wakati.

•Bryan Johnson alisema juhudi zake za kupunguza umri zimefanikiwa na akasema inaonekana amerudisha nyuma umri na inaonekana amepoteza miaka 22.

Image: BBC

Mfanyabiashara milionea, Bryan Johnson, amelipa mamilioni ya dola kubadili umri wake halisi. Bryan anataka kupunguza uzito akifikisha miaka 18.

Mwanamume huyu ambaye ni mfanyabiashara anayejishughulisha na masuala ya teknolojia, anafanya jambo ambalo baadhi ya watu wameeleza kama kutaka kurudisha nyuma saa na wakati.

"Ninajaribu kuwa kama kijana mdogo wa umri wa miaka 18," Bw Johnson alisema.

Alisema kuwa mtoto wake ana umri wa miaka 17 na anashindana naye na anataka wafanane na kiumri.

“Mwanangu ana umri wa miaka 17 na huwa nataniana naye kila mara na kusema nikiwa mdogo nataka kuwa kama wewe,” alisema.

Bryan Johnson, aliiambia BBC, kuwa mtu anaweza kujitahidi kubadilika au kupunguza umri wake.

"Ikiwa tutakufa kwa kiwango tunachozeeka au tukirekebisha itabadilisha jinsi tunavyoonekana kama wanadamu," aliongeza.

Bryan anafanya kazi na madaktari na wanasayansi tofauti 30 juu ya mchakato wa kuzuia kuzeeka na anatumia mamilioni ya dola kuishughulikia.

Madaktari mara kwa mara hufanya vipimo na vipimo vya kupima utendaji wa viungo vya mwili.

Madaktari hawa huandika ratiba yake ya kila siku na tabia yake ya kawaida kama vile chakula na nyakati zinazofaa zaidi kwake kufanya mazoezi.

“Kuna wakati huwa naamka usiku na kwenda chooni, lakini ninapofanya hivyo husababisha tatizo hili na ubora wa usingizi unapungua, kwahiyo nilileta mashine inayopima hivi,” alisema.

"Kwa kweli daima kuna hatari, ni muhimu pia kuwa salama," alisema

Image: BBC

Aliongeza kuwa ili asiamke usiku na kupata usingizi wa hali ya juu anatakiwa kupunguza mambo yanayoweza kusababisha mkojo kuwa mwingi mfano maji.

Bryan Johnson alisema juhudi zake za kupunguza umri zimefanikiwa na akasema inaonekana amerudisha nyuma umri na inaonekana amepoteza miaka 22.

"Tumepiga hatua hadi miaka 22 nyuma na ngozi yangu inaonekana ya zamani."

Baryan alisema kuwa wapo watu wanaomuunga mkono katika vita vyake dhidi ya uzee, lakini pia kuna watu wanaomkosoa na kumpinga.

“Kuna watu wachache ambao wanafurahia ninachokifanya, pia kuna watu kadhaa wanachukia na ninakipenda,” alisema.

Dk Jordan Shalain anaamini kwamba ni juu ya mtu binafsi kucheza kamari na afya yake.

"Sijui kwa nini watu wanataka kucheza kamari na afya zao. Ikiwa dawa ni nzuri kama vitamini, wewe pia unacheza kamari na pesa zako," alisema Dk Jordan.

Kwa upande wake Bryan Johnson, anasema huenda kukawa na hatari kutokana na hatua alizochukua.