Usambazaji wa mali Kenya: Takwimu na idadi za 2023

Uafikiaji wa elimu bora na vifaa vya mafunzo kwa watu huwapa maarifa na ujuzi muhimu katika ufanisi wa soko la kazi na kuzalisha mali.

Muhtasari
  • Huwa umewekwa katika kikundi cha asilimia moja katika mali iwapo mali yako kwa ujumla inaafiki kima cha shilingi milioni 16.3 au Dola 119000 kulingana na Forexbrokers.co.ke.

Katika Kenya, usambazaji wa mali umekumbwa na sifa ya kitengo kati ya matajiri na maskini. Kulingana na Benki ya Ulimwengu idadi ya watu asilimia 10 wanamiliki asilimia 42 ya mali yote nchini , wakati ambapo kiwango cha chini asilimia 40 wanamiliki chini ya asilimia 1.

Huwa umewekwa katika kikundi cha asilimia moja katika mali iwapo mali yako kwa ujumla inaafiki kima cha shilingi milioni 16.3 au Dola 119000 kulingana na Forexbrokers.co.ke.

Kutofautiana huku kwa usambazaji wa mali  kunaweza kuchangia matatizo ya kunawiri kwa uchumi, usawa na utulivu wa kijamii pamoja na kuafikia huduma muhimu kama vile afya na elimu. Ni muhimu kutathmini sababu zinazosababisha kutofautiana kwa usambazaji wa mali.

1. Sababu zinazoathiri mkusanyikoko la mali

Sababu ambazo huchangia mkusanyiko wa mali Kenya.Kuelewa sababu hizi ni muhimu kuchambua nafasi ya uchumi na matatizo yanayowakumba  watu wanapotafuta kupenya katika kategoria ya asilimia moja ya utajiri.

Kukua kwa uchumi na nafasi huchangia  pakubwa katika mkusanyiko wa mali. Uchumi unaoshamiri katika vitengo vingi vya kuekeza  huchangia hali nzuri ya watu kuyakusanya mali. 

Kwa kuongeza, mazingira mazuri ya kibiashara  pamoja na sheria zinazounga mkono wafanya biashara na uvumbuzi huchangia pakubwa ongezeko la mali. Mendeleo katika elimu na ujuzi pia ni muhimu  kunawirisha uchumi.

Uafikiaji wa elimu bora na vifaa vya mafunzo kwa watu huwapa maarifa na ujuzi muhimu katika ufanisi  wa soko la kazi na kuzalisha mali.

Kuekeza katika elimu, mafunzo ya kiufundi na ujuzi zaweza kusababisha mapato ya mtu katika hela na ufanisi kwa muda mrefu.Kuziafikia rasilimali na mtaji ni sababu nyingine.

Kutofautiana katika huduma za kifedha, mkopo na nafasi za kuekeza kukwaza usambazaji wa mali kwa watu katika rasilimali finyu.Kuunganisha au kujaza pengo hili pamoja na kukuza huduma za kifedha huweza kuchangia uundaji wa mali miongoni mwa watu wengi.

2. Gharama ya maisha Kenya

Hili kuangazia pesa zinazohitajika ndipo kuwepo katika asilimia moja ya watu wenye mali nchini kenya, ni muhimu kuangazia gharama ya maisha katika taifa.

Gharama ya maisha hutofautiana  iwapo mmoja anaishi mjini au vijijini.Katika eneno la mji,kwa mfano  Nairobi,mji mkuu,gharama ya maisha huwa ya juu sana ikilinganishwa na kule kijijini.Gharama za nyumba,usafiri,afya na elimu uchangia pakubwa ujumla wa gharama za kimaisha.

Nyumba nchini Kenya yaweza kugharamu kutegea ni ya aina gani au iko wapi.Katikati ya mji ,kodi huwa ya juu ila vijijini hutoa nyumba ambazo watu humudu. Gharama za usafiri ,mafuta na ada katika usafiri wa umma na utunzaji wa magari ni baadhi ya gharama.

Gharama za kiafya hasa bima ya matibabu, miadi ya daktari na matibabu yenyewe pia vinaweza kusababisha gharama ya maisha. Ada za elimu kama vile karo ya shule na vingine vinavyohusishwa na elimu, pia zinapaswa kuangziwa hasa katika fmilia zenye watoto.

3. Kizingiti cha kuhesabu asilimia moja ya utajiri

Kizingiti cha kuhesabu  namba kamili ya umiliki wa asilimia moja ya mali kunahitaji kuchambua mapato na utafiti deta ya  mali.

Baadhi ya mbinu zilizopo katika sababu hii,ni kama vile deta za ushuru katika mapato, kuchunguza mali na mbinu zingine za kuangazia uchumi.Ndipo kukiangazia kizingiti, wanatakwimu na wanauchumi huangazia mifumo ya usanbazaji wa mali katika taifa.

Huangazia maswala kama kitengo cha mapato, hushikiliaji wa mali pamoja na usambazaji wa mali. Katika uchambuzi huu,wanaweza wakavumbua kiwango cha mapato au thamani ya ujumla kile ambacho kinahitajika ndipo kuwepo kwa asilimia mija ya utajiri.

4. Asilimia moja ya utajiri Kenya

Huangazia sifa za idadi ya ya watu wanaotajwa kma asilimia moja ya matajiri pia ni tofauti. Watu katika kategoria hii huwa na usuli  wa aina aina ,kama vile wenyeji wa biashara,wanabiashara wakubwa,wataalamu na waekezaji. Viwanda kama masuala ya kifedha, mali isiyohamishika,keknolojia na viwanda vingine huchangia mkusanyiko wa mali.

Ni muhimu kufahamu kuwa, asilimia moja wa utajiri katika kategoria huwa si fasta.Kwa muda, watu wanaweza wakapenya au kutoka katika kitengo hiki kadri mapato yao au utajiri unavyobadilika. Suala la uchumi na uekezaji pamoja na mapato ya kibinafsi huwa na nafasi katika kudumisha au kuafikiana na kitengo cha mali.