Kimemramba: Ruto amgeuzia Mudavadi ombi lake kununulia shule basi, "wewe nunua tu!"

Mudavadi alikuwa amemuomba Ruto kuchangia katika kuinunulia Shule ya Nairobi School basi jipya lakini Ruto akamgeuzia na kumtaka Mudavadi kulinunua basi hilo mwenyewe.

Muhtasari

• Viongozi hao walijumuika na mamia ya wengine katika hafla ya uzinduzi wa bweni jipya pamoja pia na kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya jengo jipya.

DP Ruto awasili Bomas katika uzinduzi wa azma ya urais wa Mudavadi
Image: Ezekiel Aming'a

Mnamo Alhamisi, Mei 25, 2023, Rais William Ruto alijiunga na Shule ya Nairobi katika kuanzisha bweni jipya na kuweka jiwe la msingi la jengo jipya la Maabara ya Sayansi katika shule ya upili ya daraja la juu.

Aliandamana na wahitimu kadhaa wa Shule ya Nairobi, akiwemo Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, na wanasiasa wengine wengi.

Kabla ya kumkaribisha Rais Ruto kutoa matamshi yake, PCS Mudavadi alimwomba Rais Ruto kununua basi la shule kwa shule hiyo.

"Kwa kweli huu ni wakati wa unyenyekevu kwangu. Mheshimiwa rais, nilijiunga na Shule ya Nairobi mwaka wa 1974 kisha nikatoka nje ya milango mwaka wa 1979. Hiyo ni miaka 44 leo. Kwa hivyo leo niko hapa, nikifurahi sana kwamba tulirudishwa ndani ya shule hii na kuingia na kutazama majengo, nyakati hizo nzuri zilirudi," PCS Mudavadi alianza.

Mkuu wa mawaziri aliendelea na kusema kuwa alikuwa radhi kutoa shilingi milioni moja kwa ajili ya shule hiyo kupata basi jipya ili wasipate aibu wanapotembelea shule zingine na kumuomba Ruto kuchangia katika kufanikisha kununuliwa kwa basi hilo.

Hata hivyo katika kujibu kwake, rais Ruto alimtaka Mudavadi kutotoa mchango bali kununua basi mazima kwa ajili ya shule hiyo, huku akionekana kukwepa ombi la kutkiwa kuchangia katika ununuzi wa basi hilo.

“Nataka kuweka pingamizi juu ya kile alichosema Mudavadi kuhusu basi. Nadhani, mkuu wa mawaziri Mudavadi, nunua tu basi. Na ikiwa unahitaji kutafuta marafiki, na mmoja wao amesimama mbele yako. Kwa hivyo, nina uhakika Musalia atatoa basi. Kwa hivyo angalau tumeondoa jambo moja kwenye orodha ya mambo mengi yaliyoitishwa,” Rais Ruto aliambia umati uliojaa watu akijibu alipokuwa akitoa hotuba yake.

Hii hapa video ikionesha jinsi Ruto alijibu Mudavadi kwa ujanja wa sungura.