Niliomba Uhuru Kenyatta msamaha- Rais Ruto asema

Haya yanajiri huku waziri mkuu wa zamani Raila Amollo Odinga akikataa kuhudhuria maombi ya kitaifa

Muhtasari
  • Katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana, rais Uhuru Kenyatta na  Rais wa sasa William Ruto hawakuwa wakionana ana kwa ana.
ametetea mswada wa fedha wa 2023.
Rais Ruto ametetea mswada wa fedha wa 2023.
Image: Facebook

Rais William Ruto amesema aliomba msamaha kutoka kwa mtangulizi wake Uhuru Kenyatta wakati wa Maombi ya Kitaifa mwaka jana.

Akiongea wakati wa mkutano wa maombi ya Kitaifa uliofanyika katika uwanja wa Safari Park siku ya Jumatano, Ruto alisema ni sadfa kwamba mada ya mwaka huu ni kuhusu upatanisho.

“Nakumbuka wakati wa kiamsha kinywa cha maombi ya 2022 nilikuwa nikiomba msamaha kutoka kwa rafiki yangu aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta, inafurahisha kwamba katika mkutano wetu wa kwanza wa maombi, tunajadili msamaha,”Amesema.

Hajawahi kusema kwamba ni muhimu kwa viongozi kukumbatia maridhiano na daima kufanyia kazi msamaha ili taifa lisonge mbele.

Katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana, rais Uhuru Kenyatta na  Rais wa sasa William Ruto hawakuwa wakionana ana kwa ana.

Uhueu Kenyatta alionekana kuwa na uhuiano wa karibu sana na kiongozi wa Azimio One Kenya Raila Odinga ambao ulishuhudia William Ruto akiwekwa kando sana katika serikali ile ile aliyokuwa naibu rais.

Hata hivyo amebainisha kuwa hana kinyongo na rais huyo wa zamani na kwamba yuko tayari kukumbatia mitazamo tofauti hata kutoka kwa upinzani kwani itamsaidia kila wakati kuona mambo katika mtazamo bora.

Haya yanajiri huku waziri mkuu wa zamani Raila Amollo Odinga akikataa kuhudhuria maombi ya kitaifa kutokana na kile alichokitaja kuwa mkusanyiko usio wa dhati wakati Wakenya wanateseka.