Akina mama wameumia sana kulala pekee yao-Gachagua kuhusu pombe haramu

"Nataka kwenda Nyeri kisha nitasafiri kwa ndege hadi Meru nina kongamano huko kuzungumzia kahawa

Muhtasari
  • Naibu Rais alisisitiza kuwa wanawake wanalalamika na akaagiza polisi kuwasaidia wanawake hao kwa kutokomeza pombe na bangi na kuwarudisha vijana hao majumbani mwao.
Image: DP Rigathi Gachagua

Naibu Rais Rigathi Gachagua katika eneo la Menengai Kaunti ya Nakuru hii leo amelalamika kuwa wanawake wanateseka katika eneo la Mlima Kenya kwa sababu wanaume hawatimizi haki zao za kitanda.

Alisema vijana wa kiume wanatumbukizwa katika pombe haramu wakilala kwenye mitaro na chini ya kitanda badala ya kulala kitandani na wake zao.

Naibu Rais alisisitiza kuwa wanawake wanalalamika na akaagiza polisi kuwasaidia wanawake hao kwa kutokomeza pombe na bangi na kuwarudisha vijana hao majumbani mwao.

Gachagua alisema wakati mwingine nyuma aliwaagiza Machifu na polisi kutokomeza pombe haramu katika eneo la kati na kwamba anafurahi kwa sababu amekuwa akipokea maoni ya kufurahisha kutoka kwao.

"Nataka kwenda Nyeri kisha nitasafiri kwa ndege hadi Meru nina kongamano huko kuzungumzia kahawa. Nilikuwa hapa Nakuru wakati fulani nilirudi kuzungumzia pombe haramu na bangi, niliwaagiza Machifu kutokomeza pombe haramu na Nina furaha ninapokea maoni chanya."

“Hii pombe haramu ilikuwa inaharibu vijana wetu, vijana wetu walikuwa wanalala kwenye mahandaki, wengine wameoa hivi karibuni na badala ya kulala na wake zao ili kuwazaa watoto, wanalala chini ya kitanda na wanawake wanalalamika na Unajua tunataka watoto. .Nawaomba polisi na machifu kuwasaidia wanawake hawa kwa sababu wameteseka kwa muda mrefu."

Gachagua aliendelea na kukariri kwamba Machifu wana chaguo mbili pekee; kutokomeza pombe haramu au kuacha nafasi zao kama Chifu. Aliongeza kuwa kwa vile pombe haramu haiwezi kuzungumza basi chaguo pekee ni Chifu kuondoka.

"Niliwaambia wakuu mna chaguzi mbili, katika eneo lenu na eneo dogo Chifu na haramu hawezi kukaa pamoja, lazima mmoja aende na kwa sababu pombe haiwezi kuzungumza basi Chifu atalazimika kuondoka."