UFISADI KAUNTI YA SIAYA

Kamati maalum ya bunge la kaunti Siaya yapendekeza kufurushwa kwa Naibu Gavana William Oduol

Amenunua kiti chake kinachogharimu shilingi milioni moja

Muhtasari

• Samani hiyo iliyotumika kuwakilisha iliyokuwepo inadhaniwa kugharimu million 11, huku kiti cha wahudumu wa ofisi ikimgharimu mlipa ushuru milioni moja.

• Katika shutuma hizo, wawakilishi wadi kaunti hiyo waliongeza utovu wa nidhamu kwake, ufisadi na pia kutomheshimu Gavana James Orengo.


Wakili Paul Nyamodi (kulia) na naibu gavana wa Siaya William Oduol mbele ya kamati maalum ya Bunge la Kaunti ya Siaya mnamo Juni 6, 2023. Picha: JOSIAH ODANGA
Wakili Paul Nyamodi (kulia) na naibu gavana wa Siaya William Oduol mbele ya kamati maalum ya Bunge la Kaunti ya Siaya mnamo Juni 6, 2023. Picha: JOSIAH ODANGA

Kamati maalum ya bunge la kaunti ya Siaya inayoshughulikia maendeleo ya kibiashara imempata na hatia naibu gavana wa kaunti hiyo William Oduol  na kupendekeza atimuliwe kwa madai ya ufisadi.

Kuna madai kuwa Oduol alinunua kiti chake cha ofisini kwa kima shilingi milioni moja.

Kulingana na kamati hiyo punde tu alipoingia ofisini, Oduol aliamrisha ofisi hiyo kufanyiwa marekebisho mara moja, hadi kubadilisha samani iliyokuwepo.

Samani iliyokuwepo ilibadilishwa na ambayo inadhaniwa kugharimu million 11, huku viti vya wahudumu wa ofisi vikimgharimu mlipa ushuru shilingi milioni moja.

Madai hayo kwa Oduol yamesababisha sintofahamu ambazo zimepelekea kufuatilia namna pesa za umma zilivyotumika vibaya, huku ikifahamika kwamba alikuwa akimshutumu Gavana James Orengo kwa madai ya kuhusishwa na ufisadi.

Mara ya kwanza Oduol alishutumiwa na bunge la kaunti ya Siaya wiki iliyopita shitaka hilo likiachwa mikononi mwa Seneti ndipo kubaini hatma yake.

Katika shutuma hizo, wawakilishi wadi wa kaunti hiyo waliongeza  utovu wa nidhamu kwake, ufisadi na pia kutomheshimu Gavana James Orengo ambaye ni rafiki wa karibu wa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.