OMONDI AMSHUTUMU RUTO

Mungu aliwapa maji na chakula kwanza Adam and Eve - Eric Omondi

Rais Ruto alituahidi maisha mazuri na rahisi, angalia bei ya unga na sukari sasa!

Muhtasari

•Hakuna mtu ambaye hana kwa kuishi, hata mjomba wangu mwenyewe anayeishi katika vibanda vya Kibera, anachohitaji sasa hivi ni chakula na maji.

•Rais mwenyewe alizungumzia kumhusu mama mboga na mtu wa bodaboda, mimi binafsi nimekatwa mara nne, nimekutana na watu wa bodaboda huko ambao wamekamatwa kwa makosa madogo sana.

Muigizaji Eric Omondi avamia serikali ya Kenya Kwanza
Muigizaji Eric Omondi avamia serikali ya Kenya Kwanza
Image: Instagram, Facebook

Mwanablogu na muigizaji Eric Omondi amejitokeza na kuishutumu serikali tawala ya Kenya Kwanza.

Katika kikao kilichoandaliwa na RMS Jumatano usiku, Omondi alikuwa mmoja wa waalikwa waliopinga sana sera hiyo ya serikali ya ujenzi wa nyumba.

Katika mahojiano Omondi alisema kwamba, mazungumzo hayo yanayohusu ujenzi wa nyumba za bei nafuu hayakupaswa kuwepo, huku Wakenya wengi kwa sasa wakilalamikia bei ghali ya bidhaa za matumizi ya kila siku hasa bei ya chakula.

Eric alieleza kuwa hata Mungu mwenyewe katika uumbaji wake aliwapa Adam na Eve maji na chakula, hata hawakuwa na nguo.

“ Nafikiri mazungumzo haya yanayohusu ujenzi wa nyumba kwa sasa ni makosa kuyazungumzia. Serikali ya Kenya Kwanza ilituahidi maisha mazuri na rahisi watakapofuzu katika uchaguzi. Rais mwenyewe alizungumzia kumhusu mama mboga na mtu wa bodaboda, mimi binafsi nimekatwa mara nne, nimekutana na watu wa bodaboda huko ambao wamekamatwa kwa makosa madogo sana.”

Omondi aliendelea kusisitiza kuwa hakuna mtu asiye na makao. Alieleza kwamba Juni 1 wakati taifa lilikuwa likisherekea maadhimisho ya siku ya madaraka ya miaka 60 raia wamekuwa na kwa kuishi kwa miaka yote hiyo.

“Hakuna mtu ambaye hana kwa kuishi, hata mjomba wangu mwenyewe anayeishi katika vibanda vya Kibera, anachohitaji sasa hivi ni chakula na maji.Kuna baadhi ya vitu binadamu hawezi kuishi bila; chakula, maji, na afya.”

Haya yanajiri huku mjadala wa ushuru wa nyumba na kupanda kwa bidhaa hasa unga ukuindelea kuibua hisia mbalimbali miongoni mwa Wakenya huku wengi wao wakionesha hisia za kutokubaliana na pendekezo hilo la serikali.