Maandamano makali yazuka Murang'a serikali ikifunga zaidi ya 70% ya vilabu vya pombe

Wito wa DP Gachagua wa vita dhidi ya ulevi Mt Kenya unaonekana kushika kasi, baada ya kusema kuwa kina mama wanalia wanaume wao hawakidhi mahitaji yao ya kimapenzi kutokana na ulevi.

Muhtasari

• Wiki jana, gavana Kang’ata alitoa vibali takribani elfu moja pekee vya leseni za baa kuhudumu katika kaunti hiyo ya Mlima Kenya.

• Vibali hivyo vilikuwa kati ya maombi takribani elfu 3 ya baa ambazo zilituma kupewa leseni za kuhudumu.

 

Mwanamke amwekea 'mchele' mwanamume kwenye baa kisha kumuibia 849k
Mwanamke amwekea 'mchele' mwanamume kwenye baa kisha kumuibia 849k
Image: Maktaba

Wamiliki wa kumbi za starehe na kuuza pombe katika kauti ya Murang’a wameandamana kulalami,ia kufungwa kwa baa zao na serikali.

Hii inakuja siku chache baada ya uongozi wa kaunti ukiongozwa na gavana Kang’ata kutangaza kupunguzwa kwa vilabu vya pombe kwa takribani asilimia 70.

Waandamanaji hao walikuwa wanalalamika kwamba mchakato wa kufutiliwa mbali kwa leseni za vilabu kuhudumu haukufanyika kwa uwazi huku pia wakisema kuwa kulikuwepo na ufisadi ambao uliona baadhi wakifungiwa baa zao na wengiwa kuachwa wakiendelea na biashara hiyo.

Kufungwa kwa baa hizo kunakuja miezi michache baada ya naibu wa Rais Rigathi Gachagua kutangaza kwamba vita dhidi ya pombe haramu katika enbeo pana na mlima Kenya vitaendelea ili kuwaokoa mamia ya vijana ambao wamepotelea katika mvinyo, katika kile alisema kuwa kina mama wamekuwa wakilia upweke kwani wanaume wao hawapo kuwakimu katika mahitaji yao ya kimapenzi.

Wiki jana, gavana Kang’ata alitoa vibali takribani elfu moja pekee vya leseni za baa kuhudumu katika kaunti hiyo ya Mlima Kenya. Vibali hivyo vilikuwa kati ya maombi takribani elfu 3 ya baa ambazo zilituma kupewa leseni za kuhudumu.

Waandamanaji hao walituhumu serikali ya kaunti kwa kile walisema kuwa mchakato huo wa kuchuja vilabu vya kuhudumu na kutupiliwa mbali leseni za vilabu vingine ulikuwa na kiza kingi na wangali bado kujua jinsi shughuli hiyo iliendeshwa.

Hata hivyo gavana Kang’ata alisema kuwa mamombi mengi ambayo yalitumwa kutaka leseni yalikataliwa kwa sababu hawakufuata mchakato uluohitajika – kutuma maombi kupitia njia ya kidijitali.