Wataalam sasa wanataka vyuo vikuu kutupilia mbali kozi za 'cetificate' na diploma

Moja ya athari kuu ambazo huenda zikashuhudiwa kwenye vyuo ni kwamba wahadhiri wengi watapoteza kazi, vyuo vitapoteza pesa nyingi za hivyo kulemaza shughuli nyingi.

Muhtasari

• Pendekezo hilo limegawanya wajumbe wa jopo kazi kwani wengine wanahoji kuwa kozi za astashahada na diploma zote ziko chini ya elimu ya juu.

Wahitimu wa chuo kikuu
Mahafali Wahitimu wa chuo kikuu
Image: THE STAR

Vyuo vikuu vinaweza kukabiliwa na pigo ikiwa pendekezo la timu ya mageuzi ya elimu ya kuziwekea taasisi kozi za digrii litapitishwa.

Kulingana na jarida la The Standard, imethibitishwa kuwa Chama cha Rais kuhusu Marekebisho ya Elimu kinataka vyuo vikuu vyote vizuiwe kufundisha kozi za diploma na cheti cha astashahada.

Kulingana na jarida hilo, Iliibuka kuwa suala hilo limegawanya wajumbe wa jopo kazi kwani wengine wanahoji kuwa kozi za astashahada na diploma zote ziko chini ya elimu ya juu.

Moja ya athari kuu ambazo huenda zikashuhudiwa kwenye vyuo ni kwamba wahadhiri wengi watapoteza kazi, vyuo vitapoteza pesa nyingi za hivyo kulemaza shughuli nyingi vyuoni ambazo zinategemea maokoto kutoka kwa koto na karo zinazolipwa na wanafunzi hao.

Itakumbukwa hii si mara ya kwanza kwa pendekezo kama hilo kutolewa kwani mwaka 2015, Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu (CUE) ilisema ingefutilia mbali mafunzo ya kozi za astashahada na diploma na kusema kuwa kozi hizo zinafaa kuwa hifadhi ya taasisi za kiufundi na vyuo vikuu kubaki tu katika kuzingatia digrii na mafunzo ya baada ya kuhitimu.

"Vyuo vikuu vitaacha kudahili wanafunzi kwa kozi za astashahada na diploma kufikia Juni 30, kulingana na Kanuni za Vyuo Vikuu 2014," afisa mkuu wa CUE David Some kipindi hicho kando ya mkutano wa mashauriano wa maafisa wa chuo kikuu jijini Nairobi.

Mwenyekiti wa TVET kipindi hicho, Wilson Ogola alisema kuwa ni vyuo vikuu vya kiufundi pekee ndivyo vingeruhusiwa kuendelea kutoa kozi za astashahada na diploma, lakini agizo hili lilionekana kutofanya kazi na sasa pendekezo hilo limerejelewa miaka 8 baadae.