UFISADI ULIOKIDHIRI

Maafisa wa trafiki wakamatwa kwa madai ya ufisadi

Walikuwa wamekusanya sh. 15,820 chini ya saa 2 kabla ya kukamatwa kwao

Muhtasari

•Wakati tuliwakamata, maafisa wanne wa polisi kitengo cha trafiki walikuwa wamekusanya kima cha shilingi 15,820 chini ya saa 2. Pesa hizo zilikuwa katika noti za 50,100, na 200.

•Washukiwa hao walifikishwa katika kituo cha polisi cha EACC Integrity Centre, ambapo waliulizwa maswali kabla ya kuachiliwa. Wanne hao waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 10,000 huku uchunguzi zaidi ukiendelezwa.

Afisaa wa Trafiki akielekeza magari katika barabara kuu ya Mombasa Road jijini Nairobi
Afisaa wa Trafiki akielekeza magari katika barabara kuu ya Mombasa Road jijini Nairobi
Image: Twitter// Picha Afisaa wa Trafiki

Maafisa wanne wa trafiki katika eneo la Outering Road jijini Nairobi wamekatwa kwa madai ya ufisadi.

Kulingana na ujumbe uliotolewa na tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC, Jumatano wanne hao walituhumiwa kwa kuwahaingaisha waendeshaji magari na kuchukua hongo. Kulingana na tume hiyo, maafisa hao walikuwa wamekusanya shilingi 15,820 kabla ya kuwafumania.

“At the time of the arrest, the four traffic officers had collected a total of Ksh 15,820 in less than 2 hours. The money was largely in the denominations of 50, 100 and 200 notes,” EACC waliposti katika mtandao wa Twitter; ambayo katika tafsiri, wakati tuliwakamata, maafisa wanne wa polisi kitengo cha trafiki walikuwa wamekusanya kima cha shilingi 15,820 chini ya saa 2. Pesa hizo zilikuwa katika noti za 50,100, na 200.

 Maafisa wa idara ya upelelezi wanadai kuwakamata wanne hao, baada ya kupokea malalamishi mengi kutoka kwa madereva na baadhi ya watu wanaotumia barabara hiyo.

“EACC undertook this operation following numerous complaints from motorists and members of the public who alleged that of late, they have consistently witnessed traffic police officers openly collecting bribes from private and public service vehicles,” Kauli hiyo iliendelea. EACC ilichukua jukumu la oparesheni hiyo, baada ya kupokea malalamishi kutoka kwa waendeshaji magari na raia wengine walioripoti madai hayo, ambapo walisema kuwa, walishuhudia maafisa hao wa polisi wakichukua hongo hadharani katika magari ya kibinafsi na magari ya umma.

Kulingana na kauli iliyotolewa na tume hiyo, baadhi ya madereva walivumbua njia za kuwapa askari wa trafiki pesa, ambapo wanaweka pahali spesheli nje ya magari yao. Wengine, huwachilia noti hizo chini, ambapo maafisa huziokota.

Katika kesi nyingine, madereva huweka pesa ndani ya mifuko ya leseni zao za magari, ambapo askari huona na kuzichukua wanapowakabidhi leseni hizo kuzikagua.

Washukiwa hao walifikishwa katika kituo cha polisi cha EACC Integrity Centre, ambapo waliulizwa maswali kabla ya kuachiliwa. Wanne hao waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 10,000 kila mmoja, huku uchunguzi zaidi ukiendelezwa.

Haya yanajiri wakati ambapo, mjadala unaendeshwa bungeni kuhusu mswada tata wa fedha mwaka wa 2023, ambapo baadhi ya wabunge wanapinga pendekezo la mswada huo wakisema kuwa, ufisadi umekidhiri nchini ilhali wakenya wanaendelea kutozwa ushuru.