Mauaji ya Shakahola

Waumini wa Mackenzie waanguka mbele ya Mahakama, Shanzu

Mackenzie na Msaidizi wake Mwakalama, wanaendelea kula chochote wanachopewa gerezani

Muhtasari

• Mkuu wa mashtaka Jami Yamina anasema kuwa miongoni mwa washukiwa hao,  16  walisusia kula kwa kipindi cha siku 10.

 

Wafuasi wa mhubiri wa dhehebu  la Good News International, waomenekana kuwa na udhoofu katika afya, huku wengine wakianguka mbele ya mahakama ya Shanzu.

Waumini hao walilemewa kufika mbele ya mahakama Jumatano 14, kujibu mashtaka dhidi yao ambapo wameshtakiwa kwa tuhuma za kujaribu kujiua.

Washukiwa 18 pamoja na mkewe Rhodha Mumbua walifikishwa mahakamani, ili kubaini iwapo wataachiliwa au wataendelea kuzuiliwa, hata hivyo, walipokuwa wakiongozwa kwenye gari la polisi, wengine wao walishindwa kutembea, huku mmoja wa wanaume hao akianguka chini na kushindwa kuamka kwa udhoofu wa mwili wake.

Mkuu wa mashtaka Jami Yamina anasema kuwa miongoni mwa washukiwa hao,  16  walisusia kula kwa kipindi cha siku 10.

Hata hivyo, kiongozi wao Pastor Paul Mackenzie na msaidizi wake Smart Mwakalama wamekuwa wakila chochote walichopewa wakiwa rumande.  Wiki chache zilizopita  Mackenzie aliomba kununuliwa mkate.

“Tunahofia kuwa baadhi watapoteza maisha yao wakiwa korokoni. Wengine wamekataa kula au kunywa maji kwa kipindi cha siku 10. Tutaongelelea hili maana hatujui iwapo watakuwa hai kufikia kesho.” Alisema Yamina.

Haya yanajiri huku mkuu wa mashtaka ya umma akieleza kuwa, wafuasi wa Mackenzie watafanyiwa uchunguzi wa akili licha yao kushikilia imani yao ya kufunga kula na kunywa ili wamuone  Mungu. Alisema pia watalazimishwa kula. 

Kulingana na maovu yaliyoendelezwa na mhubiri huyo tatanishi Paul Mackenzie, waziri wa usalama Prof. Kithure Kindiki alisema kuwa mhubiri huyo atasalia jela hadi kifo chake. Hili lilichangia mkewe Mackenzie kutishia kwamba, naye ataendelea kukaa njaa akiwa jela.

Mhubiri Mackenzie aliendelea kusema kuwa, hajapata haki licha ya mahakama kubaini hatma yake mbele ya mahakama.