MSWADA WA FEDHA

Jeremiah Kioni: Alfajiri mpya inakuja, Tukutane Jumanne

Njia ya kulazimisha na kupitisha mswada wa fedha, ni kuturudisha kwenye siku za awali za giza

Muhtasari

•Kulingana na mswada huo, Wakenya wanatarajiwa kupunguziwa mapato yao kwa kiasi kikubwa, huku wakikumbwa na gharama nyingine nyingi hasa katika usafiri pamoja na nishati kutokana na ushuru.

JEREMIAH KIONI
Image: ENOS TECHE

Mwanachama wa Jubilee Jeremiah Kioni, ameendelea kupinga vikali mswada wa fedha uliopitishwa na wabunge Juni 20.

Katika mtandao wake wa Twittter Kioni alisema, ukosefu wa maadili mema na utiifu katika serikali hii si kizingiti katika cheo, kwa kuwa hata miundo rahisi inapuuzwa.“It’s clear that the lack of morality and conscience in this government is not limited to rank, even the simplest structures are ignored. The forceful approach of passing the finance bill by a true minority is a way of taking us back to the dark days of the past. A new dawn is coming. Tukutane Tuesday.” Alikiri.

Ambayo yanatafsiriwa kuwa; Ni wazi kwamba ukosefu wa maadili na dhamiri katika serikali hii si kizingiti kwa cheo, hata miundo rahisi hupuuzwa. Njia ya kulazimisha ya kupitisha mswada wa fedha dhidi ya waungwana wachache ni njia ya kuturudisha kwenye siku za giza za zamani. Alfajiri mpya inakuja. Tukutane Jumanne.

Kulingana na mswada huo, Wakenya wanatarajiwa kupunguziwa mapato yao kwa kiasi kikubwa, huku wakikumbwa na gharama nyingine nyingi hasa katika usafiri pamoja na nishati kutokana na ushuru.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya muungano wa Azimio la Umoja kuandaa kikao na wanahabari, ambapo kiongozi wa NARC Kenya Martha Karua aliweka bayana kuwa Jumanne wiki ijayo katika uwanja wa Kamukunji, wataweza kubaini mstakabali wao kuhusu mswada uliopitishwa.

Kulingana na viongozi wa upinzani, wanakiri kuwa mswada huo ulipitishwa kwa lazima ambapo wengine walisema kuwa Rais aliwahonga wabunge kuupitisha kwa manufaa yao wenyewe madai aliyokana Rais Ruto.