TUTANGENEZA KAZI PAMOJA

Sitaki niwadanganye kwamba tuna kazi zenu - DP Gachagua kwa wahitimu

Serikali haitawatengenezea nafasi za ajira, mtaisaidia kutengeneza

Muhtasari
  • Wabunge wetu katika bunge la kitaifa kwa usiku mbili walipitisha mswada wa fedha, wenye ushuru wa nyumba.
  • Nyumba 200,000 zinapaniwa kujengwa kila mwaka. Katika nyumba hizo chuo hiki kitatoa wahadisi wa ujenzi, mafundi wa mifereji ya maji, wakaguzi wa ardhi katika ujenzi, na utapata nafasi ya kuishi.
Naibu Rais akihutubia wanafunzi waliohitimu chuo kikuu cha JKUAT Juni 23
Image: TWITTER

Naibu Rais Rigathi Gachagua amewaeleza bayana wanafunzi wanaotazamia kufuzu kwa nyanja mbalimbali za kazi katika chuo kikuu cha JKUAT, kuwa hataki awadanganye kwamba serikali itawatengenezea nafasi za ajira.

Badala yake, Gachagua alisema kuwa kupitia ushuru unaolengwa kukatwa kwa Wakenya kuanzia mwezi ujao, kugharamia mradi wa serikali wa kujenga nyumba kwamba hapo ndipo kuna nafasi za ajira.

Ooh, mnasema mambo ya job, eeh? Hapo iko kibarua. Am an honest man. I dont want to sit here and lie to you that we have jobs for you, these jobs we are going to create them together with you. This is a University of science and technology. Our members of the National Assembly, very crescively for two nights passed the financial bill, create a housing fund to construct 200,000 houses every year. Among those houses in this university, there will be architects, there will be building engineers, quantity surveyors, plumbers and you will have an opportunity to earn a living.” Gachagua alisema.

Ambayo katika tafsiri; Mimi ni mtu msema ukweli. Sitaki nikae hapa niwadanganye kuwa tuna kazi kwenu. Hizi kazi tutazitengeneza pamoja nanyi. Chuo hiki ni chuo cha sayansi na teknolojia. Wabunge wetu katika bunge la kitaifa kwa usiku mbili walipitisha mswada wa fedha, wenye ushuru wa nyumba. Nyumba 200,000 zinapaniwa kujengwa kila mwaka. Katika nyumba hizo chuo hiki kitatoa wahadisi wa ujenzi, mafundi wa mifereji ya maji, wakaguzi wa ardhi katika ujenzi, na utapata nafasi ya kuishi.

Gachagua pia katika hotuba yake, alivamia vyombo vya habari nchini ambapo alisema kuwa anataka viongozi katika serikali pia waanze kushutumu vyombo vya habari kwa yale yanayofanywa yasiyofaa.

Alipigia debe kauli ya waziri wa biashara Moses Kuria, ambapo alitoka kauli iwapo kuna jambo jema kwake pia vyombo vya habari vitakuwa vyema.

"Sasa Moses Kuria amewauliza maswali tatu na wewe unalia kabisa. Hamjaona lolote. Tunataka kuwaomba viongozi wa nchi hii waungane na Moses Kuria kuwawajibisha wanahabari.

"Lazima wawajibike kwa kile wanachoandika na wanachosema na wakiandika uwongo, ni lazima wakabiliwe na ukweli. Hakuna mtu ambaye hawezi kuwajibika," Gachagua alisema.