Mbunge Salasya amuonya Miguna dhidi ya kumshambulia Babu Owino

Alisema shambulio lolote dhidi ya Babu Owino na Miguna Miguna ni dharau kwa watu wa Nairobi. .

Muhtasari
  • Salasya alisema kuwa wakati fulani Miguna Miguna alimwita mpuuzi na anafaa kuacha kuwashambulia viongozi vijana.
Mbunge Salasya azungumza sababu za kutonyoa nywele
Mbunge Salasya azungumza sababu za kutonyoa nywele
Image: Screengrab

Mbunge Peter Salasya na Babu Owino walizika ugomvi wao kwenye kaburi la sahau walijumuika na profesa Wajackoyah baada ya mkutano wa Jumatano wa Kamukunji.

Walijadiliana na kushirikishana mambo mengi kati yao na wakafurahi.

Salasya kisha akachukua fursa hiyo kumtetea Babu Owino kutokana na mashambulizi ya Miguna Miguna na kusema kuwa Azimio wameungana zaidi kuliko hapo awali.

Alisema shambulio lolote dhidi ya Babu Owino na Miguna Miguna ni dharau kwa watu wa Nairobi. .

Salasya alisema kuwa wakati fulani Miguna Miguna alimwita mpuuzi na anafaa kuacha kuwashambulia viongozi vijana.

Salasya amekuwa na sauti nyingi na wakati fulani pia alikuwa na vita mtandaoni na Babu Owino kuhusu cheo cha wabunge.

“Timu ya Azimio tumeungana zaidi kuliko hapo awali .Shambulio lolote kwa Mh@HEBabuOwino Gavana katika kutengeneza nairobi na aliyekuwa Mgombea kiti cha ugavana Nairobi @MigunaMiguna ni tusi kwa watu wa Nairobi .Miguna aliniita wakati fulani mjinga wa kipekee acha kuwashambulia viongozi vijana."

Babu Owino na Miguna Miguna wamekuwa wakishambuliana mitandaoni na vita vikachukua mkondo mwingine pale Miguna Miguna aliposema kuwa Babu Owino anafaa kudhulumiwa.

Hi ni baada ya DJ Evolve wiki jana kusema kwamba hakumuona Babu Owino akiwa na bunduki, wakatin alipopigwa risasi.